Kwanza karibu sana JF, Maana inaonekana umejiunga jana tu tarehe 16 March na hii inaonesha katika pitapita yako street ukakutana na ushauri kuwa ukiingia JF unaeza saidika, thats true!
Nirudi kwenye swala lako, bila shaka ushaingia kwenye govt payroll, Govt na baadhi ya taasisi za fedha wamekubalia katika group loan scheme ambayo wewe unahusika, lakini utaweza kukopesheka endapo utakuwa na salary slip tatu recent, hiyo ina maana kuwa kwa sasa wewe hata kama umepokea mishahara haijafika mitatu, na nijuavyo salary slip ya mshahara wa mwezi 3 utaupata kwenye mshahara wa mwezi wa 4, huletwa ofisini kwenu zikiwa na payrol za mshahara wa mwezi husika.
hata hivyo katika kipindi hicho kuna baadhi waajiri wanaweza kukataa kupisha fomu yako ya maombi ya mkopo kwa sababi katika kipindi hiki kisheria upo kwenye miezi 6 ya muda wa uangalizi yaani probation period.
Unachoweza saidika ni kitu inaitwa advance salary kutoka kwa mwajiri wako lakini hii inategemea financial position ya ofisi yako ingawa nayo haitolewi mara nyingi advantage ni kuwa haina riba.
Nakushauri uende kwenye mabank zaidi kuliko taasisi zingine za fedha kwa sababu zipo taasisi ndogondogo zilizoliza wengi hasa walimu waliokwenda kichwa kichwa.
Asante