Moment of silent
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 855
- 1,483
Habari za mda huu waungwana,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.
Nimekuwa nikisumbuka sana juu ya laini yangu ya tigo kutopatikana na iko hewani.
Watu tofauti walipokuwa wakinipigia walikuwa wakipewa ujumbe huu.''Namba unayopiga haipatikani kwa sasa"
Cha kushangaza Mnara unasoma na line iko hewani.
Nilipojaribu kuwapigia tigo huduma kwa wateja wakaniambia nipige namba hii #35*0000# ili niondoshe hiyo blockage tatizo likaondoka, kila mtu akawa akinipigia ananipata, ila cha kushangaza zikipita kama siku mbili tatizo linajirudia tena kwa kutopatikana hadi nipige hizo code number hapo juu ndio tatizo hilo huondoka.
Ukizingatia hii ni line yangu kongwe namaanisha natumia mda mrefu na pia imesajiliwa kwa majina yangu kwa kitambulisho changu cha NIDA.
Natumia line nyengine ya Vodacom kama ya ziada hii haina tatizo lolote, so ikitokea watu wa nyumbani hawanipati kwa line yangu kongwe, ndio huwa wananipigia kwa line yangu ya vodacom.
Kwa upande flani mimi ni mtafutaji ajira na unakuta sometimes katika CV zangu nimeweka namba yangu ya tigo, hivyo sometimes naona kama inanikosesha fursa, kwa kufikri kuwa nikipigiwa sipatikani.
Ijapokuwa kwa sasa katika Cv zangu huwa naweka namba yangu hii ya Vodacom.
Kwahiyo nimekuja hapa kuomba msaada wa kitaalamu naamini kuna baadhi ya watu walishawahi kukutana na tatizo kama langu.
Naomba kuwasilisha.