Nahitaji msaada wa kisaikolojia niache tabia ya ulevi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Inasikitisha sana sijui ni kwanini hata nimejikuta nimekwisha tumbukia kwenye ulevi wa kutisha kwa hali niliyofikia ni hatari kwani nakunywa pombe karibu kila siku bila ya kupumzika.

Nimeshakunywa za kienyeji karibu zote, pombe kali zote na kwa sasa nimezamia kwenye bia yaani speed yangu kwa kweli sio nzuri.

Nikinywa nikalewa naanza kujisemesha kuwa Mimi siogopi cha Ukimwi wala kansa nakunywa bia nikalale sitaki mwanamke nawaachia wanywa soda.

Kiukweli naogopa kifo kinachosababishwa na unywaji wa pombe kibaya zaidi nahisi ulevi umenisababishia niwe mbali na Mungu wetu imani imeshuka sana sipati tena muda wa kumkumbuka Yesu.

Nahitaji kubadilika lakini mwenyewe nimeshindwa ndugu wameshaongea mpaka wamechoka wameamua kuniacha tu mwenyewe nifanye ninalotaka nikipata kansa au bawasili au maradhi ya pombe nipambane nayo mwenyewe.

Naomba mtaalam wa saikolojia/kiroho wa kujitolea kunisaidia anisaidie mbinu mbadala, natambua ya kwamba maamuzi ya mwisho yananihitaji Mimi binafsi nijikane lakini kama nilivyosema imekuwa ngumu NASHINDWA.[emoji26]
 
Pole sana kuna wakati tuluenda vema mpaka ukaacha kabisa! Ninini kimekusibu tena? Kumbuka ulevi wa kila siku huchosha sana figo na hupunguza kws kiwango kikubwa uwezo wa kujamiiana...

Kama bado una tumaini la kuwa fulani positively huko mbeleni basi una nafasi nzuri ya kuilinda afya yako kwasasa!
 
Hapo kwny bawasiri nimecheka Sana mzee 😄😄😄,kwani unatumia choo Cha kukaa?

Pole Sana brother,kila mlevi/mnywaji Mara nyingi anapitia situation Kama yako(regrets) pale hangover inapokua imechachamaa lkn baadae anarudia Kule Kule.

Najua hakuna kitu nimeshauri Cha maana mpk hapo,lkn jua situation yako watu wengi wanaipitia kuanzia wanyonge,mawaziri,wanyabiashara etc.Don't give up bro.
 
Kama uliweza kusimama imara na Guru Mshana Jr, na ulipo muacha ukarudi nyuma kimaadili, rudi tena kwa Mentor wako, a.k.a RABI Master Mshana Jr
 
Tushajiuliza hizi sredi unazoletaga mfululizo za ovyo zinachochewa na nini? Leo jibu limepatikana
 
Mkuu karibu Mwanza tuna kituo cha kulea wanaopitia urahibu. Ni mafunzo ya mwaka moja.
Kunakuwa na huduma ya maombi na mind transformation kozi. Kituo kiko chini ya Kanisa TAG.BMCC mwanza. Tuko malimbe karibu na chuo kikuu cha SAUT. Kwa msaada wa Mungu utaacha.
 
Jikite na bangi wewe ..... Sasa naenda mwezi wa3 nakunywa lakini jumamosi tu na kwenye masherehe.
 
 

PITIA HAPA BRO
 
Kunywa Pombe kijana ila Kumbuka kula vizuri
Pombe hainaga madhara
shida yako Ina anzia kwenye kunywa matapu tapu utaonekana wa ovyo Sana
Starehe gharama.
 
Baada ya kuacha pombe utafanya nini umewahi kujiuliza ilo,tafuta mbadala ndio ikupe nguvu ya kujitenga na pombe na pia badili marafiki
 
Soma hiki kitabu-kinaweza kukusaidia kuna mada za jinsi ya kuacha sigara,pombe,madawa ya kulevya na jinsi unavyoweza kujitibu magonjwa na matatizo mbalimbali ya kiafya. 0756625286.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…