Nahitaji msaada wa kisaikolojia niache tabia ya ulevi

Mtu ambaye hajawahi kuwa kwenye situation yako hawezi kuelewa.

Binafsi ni vita ambayo nilipigana nayo miaka mingi na shida ni kwamba nilikuwa sikubali kwamba I have a drinking problem.

Anything unachotaka kutatua lazima ukubali kwamba tatizo lipo na linakutesa. Halafu lazima you love yourself enough to ask yourself is this what am willing to put myself through?

Sababu unakuta kesho yake haupo productive katika issues zako, ume overspend, umepata matatizo labda uligombana ukaumizwa, ukaligonga gari lako...ukagombana na mpenzi wako ama amekuacha... its not really worth it.

Cha kufanya ni kuamua kwamba I will stop. Hakuna cha kupunguza... yaani ni unastop hapo hapo. Be warned kwamba kuna withdrawal symptoms mfano za kukosa usingizi, kichwa kuuma lakini lazima ujikumbushe kwanini unaachana na pombe.

Halafu sasa tafuta kitu unachokipenda kufanya halafu tumia muda wako kukifanya. Tafuta kitu ambacho kitakuingizia kipato, kitakuweka healthy na kitakuongezea maarifa flani. Tafuta hobby yako moja, igeuze kuwa side hustle.

Kumbuka ile team yako ya kulewa kuiweka pembeni kwanza. Nilikaa miezi zaidi ya 6 mbali na sehemu nilizopenda kutembelea. Until nilipojua kwamba I am now strong enough to sit anywhere and not crave for alcohol. Hii sio rahisi. Utatemwa na wana ila usijali sana. The real ones will stay.
 
Ndo maana unasema bank wamekuibia pesa kumbe unalewa Hadi unasahau miamala unayofanya. Dawa kunywa hela zote ziishe ukose hela ya kununua hata chakula hapo utaacha pombe.
 
Well said mkuu
 
Humu kuna uzi spesho kwa walevi.

Bahati mbaya sijawahi kuuingia kusoma kinachojadiliwa, i hope walevi wakongwe inafika muda wanawaambia ukweli chipukizi kwamba "Huu upuuzi is not really worth it" Nimesoma uzi wa Prof. J kulazwa kisa figo, str8 up nimeassume ni pombe kwakua ndicho kitu ambacho amekua akihusishwa nacho sana.

Mi nakumbuka kipindi kile tunakutana jukwaa la ajira na nyuzi za ajira juzi umepost stori ya mshahara so I think ni mpunga ndiyo unakupa freedom ya kua miyeyusho. It's like am saying haujazoea kua na pesa za kiwango hicho frequently so umeamua kuzitafutia matumizi even if ni matumizi miyeyusho.

Komaa utatoka.
 
Habari

Kama ukipata nafasi ya kupumzika kazi au kama umejiajiri au kama una mda wa miezi kadhaa tafuta Safari safiri mji wowote mpya kwako na huko unapokwenda jitambulishe kama sheikh au pastor .. na ukae uko hata mwaka MKUU
 
We piga gambe tu, ila jitahidi usitumie vitu vikali sana vya kuhatarisha Organs zako za mwili. with time ulevi utaona ni uduanzi tu na kuachana nao. Pia epuka marafiki ambao shughuli zao sio highly committed.
 
We piga gambe tu, ila jitahidi usitumie vitu vikali sana vya kuhatarisha Organs zako za mwili. with time ulevi utaona ni uduanzi tu na kuachana nao. Pia epuka marafiki ambao shughuli zao sio highly committed.
Ndugu yangu anahitaji msaada wa kuacha pombe na sio kubadili kinywaji.

Kuna watu pombe wanaiweza. Wana discipline nayo. Anakunywa anavyotaka, anaspend within budget, hatom*** ovyo, na kesho yake mishe anafanya kama kawaida. Kuna wengine sasa hata nidhamu ya ku control unit anazo kunywa hana.
 
Habari

Kama ukipata nafasi ya kupumzika kazi au kama umejiajiri au kama una mda wa miezi kadhaa tafuta Safari safiri mji wowote mpya kwako na huko unapokwenda jitambulishe kama sheikh au pastor .. na ukae uko hata mwaka MKUU
Kwani ukijitambulisha kama mkulima watakunywesha pombe kwa lazima?
 
Pole sana,najua hali unayopitia,addiction ni kitu kibaya sana lakini kwa Mungu hakuna kinachoshindikana chini ya Jua,nenda kwenye makanisa ya maombezi ukaombewe,wakati mwingine unaweza kusema ni tabia yako kumbe ni pepo lina kudrive uwe mlevi ili uje kuharibikiwa maisha...
 
Unapita ln Paris Club (Lindi) nikuletee dawa ya kuacha pombe?
 
Wewe Mshana na mada yako ya Walevi nayo inahamasisha ulevi.

Mimi acha ninywe tu kwa stress hizi hamna namna
 
Mpaka hapo umevishwa pepo la ulevi ndoo maana unajuta sana kuwa mlevi .umefungwa pole sana upo mkoa njoo pm nikushauli nyakati kama hizo nimepita sana .unaweza pata hela hakuna unacho fanya cha maana.asante kanifungua minyororo hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…