Nimesoma posts zote za mleta mada na nimegundua haya akipata mke mwingine watashindwana tu, kwa sababu anaamini yeye ndio kila kitu kwenye ndoa, inaonyesha ni mbabe kwa wanawake na kibaya zaidi hana roho ya msamaha (kinyume na maandiko yanayosema samehe mara sabini) . Kama mkeo kajutia aliyokufanyia, msamehe mlee mtoto wenu, kwa nini utafute mwingine? Je wewe huna dhambi?! Pia suala la kusema kuwa mwanamke mwenye mtoto anaweza kurejesha mahusiano na mzazi mwenzie kupitia mtoto ni la kipuuzi na kukosa kujiamini. By the way, choice yako hasa kwenye umri imenishangaza kidogo, mungu akikujalia ukafika miaka 55 halafu binti ndio ana kama 30yrs, kila siku si utalala presha na sukari viko juu?!!