Mama yangu mpendwa, una tatizo moja kubwa sana. Kaa chini ujiulize, ulidhani kuolewa ni hati ya kupata mtoto?? Je ulidhani kuwa kulala na mwanamume ndo siku hiyo hiyo unapata mimba?
Futa kwanza mawazo ya kupata mtoto kichwani mwako. La sivyo kinachofuata utalala na mwanamume wa kwanza utakayekutana naye. Huko ni hatari ya kuibomoa nyumba yako mwenyewe.
Mwaka mmoja tu yaani umeshafikia mahali pa kujitangaza kuwa hupati mtoto! Wengine walikaa miaka 7 na leo wananyonyesha? Tulia mama. Watoto hawaji kirahisi hivyo. Utapata mtoto na watoto ila tulia kabisa. Si kila dawa ni tiba, nyingine ni madhara.
Tiba ya kwanza ipo kwako na ya pili ni mumeo. Asianze kelele kuwa anataka mtoto. Mkikaa na kutulizana akili, mioyo ikakunjuka mtajikuta siku si nyingi mna mtoto wenyu. Kimbizana na mahospitali ukutane na daktari feki wa Muhumbili akusarambulie kwenye korido mchana peupe.
Uwe mwombaji kwani watoto ni baraka kutoka kwa Mungu wetu.