Nahitaji mtoto

Nahitaji mtoto

Status
Not open for further replies.
Mama yangu mpendwa, una tatizo moja kubwa sana. Kaa chini ujiulize, ulidhani kuolewa ni hati ya kupata mtoto?? Je ulidhani kuwa kulala na mwanamume ndo siku hiyo hiyo unapata mimba?

Futa kwanza mawazo ya kupata mtoto kichwani mwako. La sivyo kinachofuata utalala na mwanamume wa kwanza utakayekutana naye. Huko ni hatari ya kuibomoa nyumba yako mwenyewe.

Mwaka mmoja tu yaani umeshafikia mahali pa kujitangaza kuwa hupati mtoto! Wengine walikaa miaka 7 na leo wananyonyesha? Tulia mama. Watoto hawaji kirahisi hivyo. Utapata mtoto na watoto ila tulia kabisa. Si kila dawa ni tiba, nyingine ni madhara.

Tiba ya kwanza ipo kwako na ya pili ni mumeo. Asianze kelele kuwa anataka mtoto. Mkikaa na kutulizana akili, mioyo ikakunjuka mtajikuta siku si nyingi mna mtoto wenyu. Kimbizana na mahospitali ukutane na daktari feki wa Muhumbili akusarambulie kwenye korido mchana peupe.

Uwe mwombaji kwani watoto ni baraka kutoka kwa Mungu wetu.
 
nimeolewa ni mwaka na mwez mmoja sasa ila no mimba huwa hedhi yangu inavuka hata miez 3 nilishazunguka mahospital wakanipa vidonge vya majira haikusaidia nikaenda nyingine wakanipa clomid nimetumia miez 3 ila no mimba walisema eti hormone zangu zipo chini nisaidien jamani madoct nahitaj Mtoto nifanyeje

Pole. Nataka nikutie moyo mdogo wangu. Kwa Mungu kila jambo lina wakati wake. Sijui wewe una umri gani? Lakini kwa muda wa ndoa yako mpaka leo ni mwaka na nusu kwa kweli bado usikate tamaa.

Sijui unaishi mazingira ya namna gani nataka nikwambie ili kushika mimba unatakiwa uwe salama kisaikolojia no stress ukiwa free kichwani akili salama kabisa mimba utapata.

Pia hata lishe yenu wewe na mume wako ikoje isije ikawa hupiki uko bz hospital mume hali akashiba anakula vitu amvavyo havina virutubisho pia inaweza ikawa ni sababu. So jitahid mle vizuri kwa wakati tena balance diet.

Mwisho muende hospital kwa dr bingwa wa kina mama. Ni mapema mpendwa utafanikiwa.
Zaidi Mungu ndio kila kitu atakupa haja ya moyo wako mpigie goti.

Yangu ni hayo kila laheri
 
Mama yangu mpendwa, una tatizo moja kubwa sana. Kaa chini ujiulize, ulidhani kuolewa ni hati ya kupata mtoto?? Je ulidhani kuwa kulala na mwanamume ndo siku hiyo hiyo unapata mimba?
Futa kwanza mawazo ya kupata mtoto kichwani mwako. La sivyo kinachofuata utalala na mwanamume wa kwanza utakayekutana naye. Huko ni hatari ya kuibomoa nyumba yako mwenyewe.
Mwaka mmoja tu yaani umeshafikia mahali pa kujitangaza kuwa hupati mtoto! Wengine walikaa miaka 7 na leo wananyonyesha? Tulia mama. Watoto hawaji kirahisi hivyo. Utapata mtoto na watoto ila tulia kabisa. Si kila dawa ni tiba, nyingine ni madhara.
Tiba ya kwanza ipo kwako na ya pili ni mumeo. Asianze kelele kuwa anataka mtoto. Mkikaa na kutulizana akili, mioyo ikakunjuka mtajikuta siku si nyingi mna mtoto wenyu. Kimbizana na mahospitali ukutane na daktari feki wa Muhumbili akusarambulie kwenye korido mchana peupe.
Uwe mwombaji kwani watoto ni baraka kutoka kwa Mungu wetu.

amina barikiwa
 
Nenda kwa mzee maretu arusha tatizo lako litaisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom