Nahitaji mwanasaikolojia

Nahitaji mwanasaikolojia

Me too

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
7,388
Reaction score
9,333
Heshima kwenu!!!

Kiukweli nipo serious sihitaji mzaha wa kupotezeana muda.

Kwa wanasaikolojia wote mliopo humu JamiiForums nawaombeni pindi mtakapokuwa free mnisaidie tatizo langu.

Shida yangu kuu nisaidieni namna ya kumliwaza mtu aliyejichukia na kuamua kujitenga hataki kukaa na watu. Yaani ni mkali hata namna ya kumsogelea unashindwa.

Ombi kuu mnipe mbinu za kumtoa katika hali yake taratibu yaani maneno ya kumfariji vitu vya kumfanyia n.k ili atoke katika hali hiyo inaniuma sana ndugu yangu huyu kuamua kujichukia / kujitenga hata simu hapokei katu blacklist.

Msaada wenu wanasaikolojia.
 
duuh poleni sana kuna jamaa fulani hivi huku alikua ni mwana sychology ameadimika sana sijui anaitwa nani
 
pole sana, nakushauri muache mpaka pale mwenyewe atakapoamu kurudi katika hali yake, pole tena
 
Pole sana. Unaweza kuelekeza kidogo kipi kumepelekea kuwa kwenye hiyo hali?
nahisi

either anaumwa hataki tujue au ana stress sasa hali ya kuwa mkali hataki tumsogelee nimeshindwa hata pakuanzia kumuuliza au kumchunguza. ndo maana nkataka nipate walau teknic za kumuingia step by step mpaka nifanikiwe kujua tatizo lake.
kiukweli ni mkalii mno.
 
muonyeshe upendo mfanye akuzoee kisha
ningumu kumsaidia endapo tatizo lake alijulikani

pain can make you stronger or stupid
 
pole sana, nakushauri muache mpaka pale mwenyewe atakapoamu kurudi katika hali yake, pole tena
mkuu tumuache km ana stress akikaa mwenyewe na hali hiyo si atafikia hatua ya kwenda mirembe?
 
nahisi

either anaumwa hataki tujue au ana stress sasa hali ya kuwa mkali hataki tumsogelee nimeshindwa hata pakuanzia kumuuliza au kumchunguza. ndo maana nkataka nipate walau teknic za kumuingia step by step mpaka nifanikiwe kujua tatizo lake.
kiukweli ni mkalii mno.
Pole jaribu kutafuta kwanza marafiki zake uongee nao uone kama na wao kawachukia kama hapana basi hao marafiki ndiyo utatumia kuongea nao ili wampe msaada wa kimawazo.

Usilazimishe akwambie wewe tumia watu wake wa karibu ujue kwanza tatizo lake.
 
muonyeshe upendo mfanye akuzoee kisha
ningumu kumsaidia endapo tatizo lake alijulikani

pain can make you stronger or stupid
upendo utauoneshaje wakati ni mkali hasogeleki? ndo maana nalia na wanasaikolojia wanisaidie teknic za kufanikiwa kumuingia nijue tatizo.
 
Pole jaribu kutafuta kwanza marafiki zake uongee nao uone kama na wao kawachukia kama hapana basi hao marafiki ndiyo utatumia kuongea nao ili wampe msaada wa kimawazo.

Usilazimishe akwambie wewe tumia watu wake wa karibu ujue kwanza tatizo lake.
hawasiliani na marafiki zake ni mda.
 
Back
Top Bottom