Nahitaji mwekezaji tunaeweza fanya biashara pamoja kwenye idea yangu ya bidhaa 6 awepo Dar es Salaam

Nahitaji mwekezaji tunaeweza fanya biashara pamoja kwenye idea yangu ya bidhaa 6 awepo Dar es Salaam

Akili zangu hazipo sawa

Senior Member
Joined
Apr 23, 2020
Posts
160
Reaction score
119
Kama kichwa kinavosema wakuu Nahitaji mtu anaweza akawekeza Kwenye hili wazo la biashara.WAZO LENYEWE LIPO HIVI๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Lengo kubwa nikuwasaidia wauza migahawa kuendesha biashara zao hata kama hawana mtaji na lakini pia kutanua biashara zao.Ipo hivi mama ntilie anavoamka asubuhi atataka kununua mchele,unga wa ugali,unga wa ngano,mqfuta ya kula,maharage na sukari.Vipi ikitokea siku hana hata sh mia ya mtaji let's say labda matatizo yamejitokeza katumia mtaji wote na hivyo anashndwa kununua mahitaji ya mgahawani kwake.

Lengo la wazo la biashara hii ilikuwa ni kutatua changamoto hii lakini pia kuwasaidia kutanua biashara zao zaidi. Ipo hivi wazo lilikuwa linalenga kufungua biashara itakayokuwa inamuacha mama ntilie auze apate faida halafu ndo alipie bidhaa. Lakini pia kwakuwa biashara inalenga kuhudumia Namba kubwa ya wateja Mfano Dar es salaam pekee Kuna mama ntilie karibia 20 elfu kupata mtaji wa kutosha kuwahudumia idadi kubwa ya wateja inakuwa ngumu hivyo basi njia pekee nikaona nikushirikiana na wauza maduka mbali mbali wanqouza bidhaa hizo.

Sasa biashara inapataje faida?,Ipo hivi kwakuwa bidhaa tutakuwa tunaziuza kwa kuwakopesha bei ya bidhaa itakuwa juu kidgo let's say kwa sh 200 labda tofauti na bei ya dukani Mfano mama ntilie akaja kwetu akasema yeye Leo anataka unga kilo moja, mchele kilo moja ,sukari kilo moja,mqfuta lita moja na maharage kilo moja lakini sisi tunamuuzia kwa bei ya nenda katumie utulipe jioni ambayo tuseme inazidi 200 kwa kila bidhaa tofauti na bei ya dukani, mfano kwa bidhaa za hapo juu ambazo sisi tutakuwa tumechukua duka x ambalo tuna mkataba nalo kwa bei ya dukani tutakuwa na faida ya sh 1000 kwa bidhaa hizo tano juu apo kama fee ya kukopeshea itakuwa 200 kwa kila bidhaa.

Nimesema bidhaa sita hapo juu kwenye kichwa cha thread, Bidhaa zenyewe ni unga wa ngano, unga wa ugali,mchele,sukari,maharage na mqfuta ya kula kama bidhaa anzia kwa sababu karibu zote zinatumika mgahawani. Kwa Namna biashara itakavofanya kazi na namna tutakavoshirikiana na wauza maduka karibu pm wakuu.

NAKARIBISHA MAONI NA MAWAZO YA NAMNA TUNAWEZA LIWEKA HILI WAZO KITEKNOLOGIA ZAIDI
 
Kama hakuna mtaji unaohitajika na mambo ya usajili na kurasimisha kampuni ni gharama ya Sio zaidi ya Tsh. 100,000/=

Hapo vipi, bado utahitaji kufanya ubia na mtu Kwa ajili ya kuweka wazo lako katika mchakato wa kibiashara na utekelezaji?
 
Mkuu nakufata PM message hazitoki.Tafadhali nitumue whatsApp yako tuyajenge
 
Kama kichwa kinavosema wakuu Nahitaji mtu anaweza akawekeza Kwenye hili wazo la biashara.MWEKEZAJI yeye atatoa share yake kwenye kukamlisha usajili wa hii biashara tuuuu maana idea haitaki mtaji swala tuwe registred tuuu,yaani tuna TIN Namba certificate,Leseni ya biashara na jina la biashara.Halafu tunaanza kupiga kazi.Karibuni wakuuuu tufanye biashara pamoja.PM FOR MORE INFO AND CONTACTS
Unaendeleaje na forex ndugu yangu
 
Kama hakuna mtaji unaohitajika na mambo ya usajili na kurasimisha kampuni ni gharama ya Sio zaidi ya Tsh. 100,000/=

Hapo vipi, bado utahitaji kufanya ubia na mtu Kwa ajili ya kuweka wazo lako katika mchakato wa kibiashara na utekelezaji?
Ndio ninahitaji mtu nataka yeye ndo awe mmiliki mkuu
 
Kuna point moja WaTanzania hatujaifikia bado. KUTOKUWA WABINAFSI na matokeo yake hatuendelei.

Hivi mtoa mada kitu kinachokufanya ushindwe kuweka idea yako hapa ni kudhani kuwa watakuiga au? Hivi unadhani wewe ukiwa ni mtunzi wa idea fulani hata mtu akikuiga unahisi anaweza kufanya vizuri kuliko wewe? Ngoja nikutoe wasiwasi mkuu, hata watu mia 9 wakianzisha same biashara soko lipo la kutosha na wewe una advantage kwa sababu unalijua hilo wazo ndani nje.

Kuwa na amani, weka hapa wazo lako hakuna wa kukuiga na hata wakikuiga hamuwezi kumaliza soko wote kwa pamoja! Jaribu kuwa na ubunifu tu na kujali quality baaaaasi utatawala soko amini nakwambia

Tena zaidi wapo watakao kubeza hapa na wapo watakao criticise kiuzuri tu na utaambulia maboresho mawili matatu.

Ni sawa na makazini unakuta mtu anakomaa hataki kuwafundisha madogo kazi kisa anaogopa nafasi yake, ni ujinga tu na wanasahau kuwa ukiwa unamfundisha mtu kazi wewe una jifunza zaidi na zaidi na kuwa mahiri maradufu.
 
Kuna point moja WaTanzania hatujaifikia bado. KUTOKUWA WABINAFSI na matokeo yake hatuendelei.

Hivi mtoa mada kitu kinachokufanya ushindwe kuweka idea yako hapa ni kudhani kuwa watakuiga au? Hivi unadhani wewe ukiwa ni mtunzi wa idea fulani hata mtu akikuiga unahisi anaweza kufanya vizuri kuliko wewe?...
Usjali mkuuu Kuna mtu alishasema niweke hapa nilikuwa natafuta mda niandike mkuuu sio kwamba naficha๐Ÿค—
 
Back
Top Bottom