Kuwa single mother haina maana kwamba huwezi kupata mwenza wa kufanana na wewe. Ni kweli kuna "changamoto" za kuoa single mother hasa hasa kama "baba" wa mtoto yupo.
Lakini, yaliyopita yamepita, hakuna mtu asiyekuwa na jana, hakuna asiyekuwa na "historia" iwe nzuri au mbaya.
Muhimu ni kuishi kwa kuangalia yajayo na sio kuishi kwa kuangalia yaliyopita. Yaliyopita yatabakia kama "somo" ili kesho iwe bora zaidi kwa kutokurudia makosa ya jana.
Wanaume wenzangu hebu tuache kuwananga na kuwaponda "single mothers" kama vile hizo mimba walijipa wenyewe wakati miongoni mwetu sisi ndiyo chanzo au moja ya sababu ya wao kuwa "single mothers".
Well, may be miongoni mwa Wanawake wapo ambao kwa hiari yao au kwa kiburi au kwa ujinga wamekuwa single mothers lakini bado hatupaswi kuwaweka wote ndani ya kapu moja la "wakosaji" au "watu wasiofaa".
Ndege wa rangi moja huruka pamoja. Nina imani
Molina utampata wa kufanana na wewe iwe humu JF (which I likely doubt) au iwe nje ya JF , yote heri.
Binafsi siwezi kuoa "single mother", lakini, kisichonifaa mimi kinamfaa mwingine. Wazungu wana kamsemo kao; "One man's trash is another man's treasure".