Nahitaji Partner au Partners 2 Tufanye biashara ya Kuuza Kuku Pamoja

Cards Fantasy

Senior Member
Joined
Nov 3, 2016
Posts
192
Reaction score
111
Habari za Leo Wanafamilia!

Pole na Majukum, Mm naitwa Hussein, naishi Tandika Magorofan, nna miaka 34, nna mke na watoto watatu.

Nnajishughulisha na Ufugaji, utengenezaji dawa za Asili za Kuku na uuzaji wa Kuku, kwa Sasa nimejikita zaidi kwenye Kuku wa nyama kwa kuwanunua directly kwa Wafugaji wengine au sokoni, kuwapack na kuwauuza mahotelini, mabuchani au kwenye migahawa kwa taratibu za kulipana on delivery au on credit ambapo wengi hupenda style hii.

Kutokana na kuongezeka kwa soko, na wateja wakubwa wakibaki wale wa credit imenilazimu kusaka mshirika wa kufanya nae hii biashara ili tugawane kwa kile kinachopatikana.

Mshirika atakuja kuongeza nguvu ya freezer mbili na capital ya kununua Kuku wastani 400 kila week. Ambapo nakusudia kuwe na collection point maeneo ya Kigambon, maana ukanda ule nao umebarikiwa Wafugaji wengi na nimeishi kule kipindi nafuga maeneo ya Dege.

Kwa wastani Mshirika atapaswa kuwa na capital ya Tsh Mil 3.5 Hadi Mil 5. Au wakipatikana Wawili itakuwa vzr zaidi kila mmoja atachangia pale mkono wake utakapoweza jikuna.

Wastani wa faida kwa mwezi tukitoa gharama za uendeshaji ni 10% ya capital ya kila Mshirika. Tunaweza fanya contract ya miezi 6 na kuendelea kulingana na mapenzi ya Mshirika.

Unaweza chukua capital yako kwa kutoa notice ya siku 30 kabla ili kwa mwezi husika usiwe included kwenye mgao wa faida.

Naimani mengine tutayaweka sawa pindi tukikaa mezani.

Natanguliza Shukran Sana.

Kwa mawasiliano Zaidi,

0784 645 900
0624 7400 12

Unaweza pitia fb na Instagram kwa Kukucaretz na Sokoni fresh Tz.









 
Mkuu nakukubali sana, we ni mpambanaji haswa. Kwa wakati huu ntashindwa ku partner nawe coz akiba yangu haifiki hata 2m. Mungu akijaalia huko mbele tutashirikiana
Shukran Sana brother! Asante kwa kwa kunipa Strength ya kuzidi kupambana. Nakuombea nawe huko mambo yazidi kuwa sawa kwenye harakati zako.

Karibu na Kila la kheri Sana!
 
Kuku ni wa nyama, Broiler Hawa. Wa kienyeji nafanya kwa special order.

Faida Ina range kwenye laki 5-1M kulingana na mzunguko na capital ya mwezi husika iliyokuwa inserted.

That's why naimani uwezekano wa partner kupata 10% profit ya capital yake upo.

 

Tanzania partnership? Doesn’t work, dunduliza, kuwa taratibu!
 
Wazo zuri sana ni ndoto yangu kuu sana kufanya hiii ishu ingawa tu hela ndio tatizo kwangu
Usijali Brother. Karibu tubadilishane uzoefu ukiwa na wasaa. Na Mola atakujaalia utapata capital.
 
Wewe hapo kwa sasa una mtaji wa kiasi gani? Maana umetoa kiwango tu cha kuchangia partner... Na kwa sasa wapata faida kiasi gani.
 
Wewe hapo kwa sasa una mtaji wa kiasi gani? Maana umetoa kiwango tu cha kuchangia partner... Na kwa sasa wapata faida kiasi gani.
Nilikuwa na mtaji cash Mil 4.5. Nimefanya matumizi na kubakiwa na cash ya mzunguko 1.5M.

Matumizi.

Freezer 2. 800,000/-
Pikipiki 1. 1,300,000/-
Baiskel. 1. 150,000/-
Kodi. 600,000/-
Mizan n.k. 200,000/-

Total. 3,050,000/-

Wastan wa faida kwa mwezi ni Tsh 450,000- 600,000/-.
 
Sasa inakuaje mimi nikikupa hiyo pesa 3.5m bila kushiriki direct nawewe? Ila kwa kugawana hiyo faida, na staki ribah, Security ya pesa yangu itakua je? Cikujui unijui,
 
Sasa inakuaje mimi nikikupa hiyo pesa 3.5m bila kushiriki direct nawewe? Ila kwa kugawana hiyo faida, na staki ribah, Security ya pesa yangu itakua je? Cikujui unijui,
Karibu Sana.

Kwanza utakuja kuona nyumban, na ofisi yetu ndogo. Nna Wakili Wawili mmoja akiwa sister wangu naimani tuta sort vipengele vyote muhimu ku cover Hilo hitaji la trust and credibility.

Naimani tukijaaliwa kuonana na kukaa mezani, tutafanya biashara kubwa na endelevu kwa mapenzi ya Mola na hautajutia.

Pia si riba, kwa waliosoma Sheria za Islamic contracts Kuna Musharak na Mudharab, unaweza Google kuona application yake, tutakuwa tuna base humo.
 
Good Very Good...

Ukishapata Soko umemaliza kila kitu...

Ushauri kama unataka partnership sababu ya kuongeza mtaji pekee (acha tafuta hata loans au kopa kwa ndugu na jamaa) Ila kama unataka partnership ili muweze kusaidiana na uendeshaji na kukuza biashara basi its okay (ila kuliko kutafuta watu usiowajua labda ni bora kwanza ukatafuta watu ambao ulishawajua / fanya nao kazi)

All in all ukishapata soko la uhakika, mengine yatakuja...
 
Asante sana. Nikiiangalia hii text naona imebeba both intentions, Kama ulivyosema, as long as masoko yapo ni muda muafaka wa kusogea mbele Zaidi.

Shukran sana kwa mitazamo mizuri.
 
Hongera mkuu kwa kupambana. Naomba nisaidie connection ya freezer kwa bei ulotaja hapo juu. Naamini ni deep freezer.. pia ukiweza kunipa na ukubwa wake ningeshukuru sana!
 
Hongera mkuu kwa kupambana. Naomba nisaidie connection ya freezer kwa bei ulotaja hapo juu. Naamini ni deep freezer.. pia ukiweza kunipa na ukubwa wake ningeshukuru sana!
Usijali Brother, nitext nikupe maelezo ki urefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…