Nahitaji pesa Milion 68

[emoji33][emoji33][emoji33][emoji33][emoji33][emoji158][emoji158][emoji307][emoji307][emoji171][emoji171]
 
Omba ndugu zako wanaokaribia kustaafu wakukopeshe pension zao. Au nenda kwa wajenzi huru ukatoe kafara.
 
Ukishafungua hyo pub nijulishe niwe mteja wako wa kwanza
 
Sijui hata nishauri nini...Je una experience yoyote ya biashara mpaka uwe na uhakika kwamba hiyo milioni 68 itarudi? Je umewahi kufanya biashara hata ya milioni tu? Milioni 68 ni hela mingi sana kuitumbukiza kwa mtu ambaye ni novice.
 

Labda tuliangalie kwa mapana.
Biashara haramu Tanzania hazilipiwi kodi ni "criminal".
Pub anayodai yeye ni halali kwasbb biashara hiyo inalipia kodi.
Labda ninachokiangalia mimi jinsi alivyorusha jiwe gizani!
Tulichotakiwa kama wanajamvi, tusimpatie samaki(pesa/mtaji) bali tumpatie nyavu za kuvulia (mbinu) ingemsaidia sana "kutoka".
Lakini mtu "from no where" muanze kuchangishana sijui ku-share, kwa watu msiofahamiana, mwisho wake mara nyingi huwa ni mbaya.
Na kinachokosesha imani watu ni huu utapeli ulioenea kila sehemu, ambapo maeneo memgine hauwezi kudhania.
Pesa ilivyokuwa ngumu, watu wanapiga pesa kwa kila aina ya ujanja,bila hata kumuogopa Mungu.
Hata mkiwa mnafahamiana biashara nzuri ni ile ya kusimama mwenyewe.
Utakuta hakuna lawama ama kutegeana na ikikuendea vibaya unakufa na tai yako shingoni.
 
Hahahahaha,utafiti unatoa majibu
 
weka taarifa zote hapa, 68 mln , 4 years, Dhamana ya mkopo, je utamudu riba kiasi ? na marejesho @ mwezi kiasi gani ? km utaweza sh 2,750,000= mwezi x miezi 48 karibu sana na uwe na dhamana ya 100 mln
Ndg yangu ijapo umeandika kifupi nimeipenda. Kunakitu nnataka nijifunze kutoka kwako.
Yeye anahitaji mil.68/=. Sasa unaposema asikose dhamana ya mil.100/=!
Hapo imekaaje? Ninaomba ufafanuzi zaidi kwakuwa nimeona kuwa haya mambo wewe unayafahamu zaidi.
 
Unahisi kwa awamu hii mtu atakupa bure M 68.

Na mimi natafuta M 68 ukipewa nikopeshe nitakurudishia ndani ya miezi miwili.
 
Daaa miaka 4 hyo hela kwa biashara ya pub utakuwa umepata au unatutania
 
Siku zooote fursa hazionekani kama mnavyotarajia, na kama utabahatika kuiona inaonekana kama kituko tu tena cha kukimbia kabisa isipokuwa tu MJASRIAMALI ndio pekee atakae gundua kuwa hii ni FURSA,

Hakika maelezo ya mtoa mada yuko sahihi sana tu, panahitajika nyongeza tena ndogo sana kukamilisha kula kitu, tena ana kiasi fulani cha uzoefu ndio maana akagusa swala la ubia yuko tayari
 
Point Nzur thana kuna kitu nimejifunza Shukran
 
Mfano riba ya chini kabisa 40%.
68m + 27.2m = 95m.
95m ÷ siku 1460= 65,000 shs kwa siku.

Lets assume kama bia moja faida ni shs 300.
Una wafanyakazi wa 4 uwalipe 5000 kwa siku ambayo ni 20,000. Luku 20,000.
Tuchukulie kama gharama ni hizo tu.

105,000 gharama ÷ 300 faida ya chupa = 350 ÷ 24 chupa kwenye crate. Kwa hiyo unatakuwa uuze crate 14.5 kila siku ili uweze kulipa deni la watu.

Hayo ni makadirio tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…