Nahitaji pesa Milion 68

Nahitaji pesa Milion 68

We na wewe ndo wale wale tu, njaa njaa na ujanja ujanja.
Yani kila mwezi sh 2.75M x 48 ni 132M hiyo afu kakopa 68M.

Sasa mtu akope 68M arudishe 132M huoni kama una upunguani kichwani mwako?
Hahaha
 
Kwa usawa huu wa kurejesha per diem,thubutuu hizo benki zenyewe zimesitisha kutoa mikopo kisa utumbuaji umeshika kasi,labda usubiri zoezi la uhakiki liishe may be watakufikiria lakini kwa sasa imekula kwako
 
Mimi nitakupa hiyo pesa bila masharti endapo tu utaniambia ulimchagua nani awe Rais, uchaguzi uliopita?
 
weka taarifa zote hapa, 68 mln , 4 years, Dhamana ya mkopo, je utamudu riba kiasi ? na marejesho @ mwezi kiasi gani ? km utaweza sh 2,750,000= mwezi x miezi 48 karibu sana na uwe na dhamana ya 100 mln
Hayo makampuni ya kitapeli.
 
Nahis umekosea uandishi m 68 mkopo halafu huo mkopo ndio ufanye yote hayo nadhan wewe ni mgeni wa biashara
 
Mfano riba ya chini kabisa 40%.
68m + 27.2m = 95m.
95m ÷ siku 1460= 65,000 shs kwa siku.

Lets assume kama bia moja faida ni shs 300.
Una wafanyakazi wa 4 uwalipe 5000 kwa siku ambayo ni 20,000. Luku 20,000.
Tuchukulie kama gharama ni hizo tu.

105,000 gharama ÷ 300 faida ya chupa = 350 ÷ 24 chupa kwenye crate. Kwa hiyo unatakuwa uuze crate 14.5 kila siku ili uweze kulipa deni la watu.

Hayo ni makadirio tu.
Umenyumbua vizuri sanaaa mkuu
 
Umenyumbua vizuri sanaaa mkuu

Kusema ni rahisi.
Lakini ni vizuri kujaribu kuvuta picha ya uhalisia kuona kama inawezekana.

Mambo kama haya ndio tunanaga mtu anafanya biashara miaka mingi ila anaishi kwenye mazingira magumu, au hata wengine hutamka kama biashara ya kichawi.

Kumbe ni hesabu tu hazikupigwa vizuri mwanzoni.
 
Back
Top Bottom