MALKIA WA TABASAMU
Member
- May 23, 2024
- 15
- 43
Kauli hii ni ya kila asiyenazo za kukidhi japo mahitaji yake ya lazima. Kauli hii hutamkwa hata na wale wenye nazo za kukidhi ila hazijawakinaisha.
Nikisema nazihitaji, mtauliza tofauti yangu na wao ni ipi ama ni nini?
Nahitaji pesa ili niikomboe kesho inayonitafuna sana moyoni. Ningepewa jukumu juu ya kesho yangu tu, wala isingeniumiza maana kama nikishindwa nitakuwa nimeshindwa peke yangu. Jukumu ni juu ya kizazi kitakacholeta kizazi baada yetu. Nahitaji pesa nifanye ziara. Si mikoa yote Tanzania tu, wilaya, kanda, tarafa na vijiji vyote pia.
Tumejifunza imani chanzo chake ni kusikia si ndio? Je ni imani nzuri pekee? Ama kila imani chanzo chake ni hichohicho! Kama ndivyo basi, uozo tuuonao umezalishwa na kukomazwa na mapokeo na matoleo ya habari zipewazo kipaumbele.
Ningekuwa na udhibiti juu ya hilo, hakika elimu ingeanza na tasnia ya habari. Ningewaambia tu, kile kinachopigiwa chapuo sana hata kama ni kibaya hugeuka hamasa, sio kila mja ana uwezo wa kuchambua magugu kwenye ngano.
Mimi ni shahidi ya kuwa mambo mengi machafu toka kitambo yalikuwepo. Yalikosa uhuru yaliyojipa hivi sasa, kwakuwa hayakuzungumzwa hadharani. Hayakufanyiwa mzaha wala masihara. Yalipobainika kimya kimya yalizimwa ama kutoweshwa.
Pengine haki za binadamu zilimaanisha kinyume na tulivyojifunza shuleni zamani. Ama siku hizi zinatafsiri yake yenye manufaa kwa vibopa fulani. Au, au, ....napata kigugumizi juu ya hili.
Sijapendezwa na kuitumia picha hapo chini, ila uhalisia wa kile ninachokilenga uko hapo. Watu wengi wenye nafasi mbalimbali kwenye jamii wameirusha na kunena walivyoona yafaa. Wapo waliokemea, wapo waliocheka na kudhihaki, wapo walioipachika maneno yenye kuponda wazi malezi ya upande mmoja, halafu nipo mimi kama kidole kimoja kinachopambana kuua chawa.
Ni wanaume wachache tu ndio uhusika na malezi ya watoto kwa asilimia 25 hadi 100, na amini usiamini, ushiriki chini ya asilimia hizo ni mkubwa na ndio uliozoeleka karne kwa miongo. Lakini jiulize, madhara yalikuwa makubwa namna hii? Ndoa nyingi zilidumu kwa nguvu ya mwanamke ambaye mbali na kutokuwa na utambuzi juu ya haki zake za msingi zilizokosa umuhimu zama hizo, aliijua nguvu ya uwepo wa baba kwenye maisha ya watoto.
Kuna vitu zama hizi tumevitupa kushoto kwa kigezo cha haki sawa, vimeondoa kabisa hamasa ya kijinsia. Wacha nikupe mfano wa kijinga ila wenye mantiki... Kale, kikipikwa chakula baba aliwekewa sehemu zote zilizonona za mboga, iwe nyama ama samaki, iwe kuku au mboga yoyote tu, baba wa hiyo familia alihifadhiwa sehemu nono na kubwa zaidi. Kuna watoto wa kiume waliliona lile, kwa utoto wenye shauku walijiapiza wakikua wakubwa wataoa wake aina ya mama yao ili wahifadhiwe sehemu nono kama afanyiwavyo baba yao. Walijikuta wakipenda kuwa wanaume. Waliuona ukakamavu wa baba. Waliona alivyorejea nyumbani na kitoweo baada ya mawindo/uvuvi, walijiapiza kuwa kama baba yao. Naongelea watoto wa kiume.
Baadhi walisema kinyume ila kwa namna chanya. Sisemi moja kwa moja tabia zote zilizoshikiliwa na mfumo dume kandamizi' zilijenga, zipo zilizobomoa kwa upande tofauti huku zikijenga kwa upande tofauti. Mtoto wa kiume alitamani kuwa mwanaume kwa sababu alionyeshwa wazi kuwa mwanaume ni mtawala. Vipi hivi sasa? Mtoto wa kiume anakua kwa asilimia 100 mikononi mwa mama. Viatu na nguo anazojaribisha wakati wa makuzi ni vya mama yake. Kiufupi hamasa yake ya jinsia ni mama yake. Anasikiliza zile nyimbo za "I'm a strong women" na kuzikiri moyoni mwake, tutarajie nini?
Wapo wamama baadhi waliofanikiwa kukuza wanaume wa nguvu. Hawa ni wale waliojiponya na kulea wakiwa na maarifa mengi ndani ya hisia zao za kike.
Mimi ni mwanamke, naijua nguvu iliyo ndani yetu. Kutengeneza na kuharibu vimo ndani ya kile tuchaguacho kuamini.
Nikipata nyezo, nitatoa elimu ibebayo umuhimu wa malezi nitaipenyeza kwenye kila sikio la kijana wa kiume na mwanaume mtu mzima. Nitawaambia namna wao ni muhimu kweye ukombozi wa hili taifa na Afrika kwa ujumla. Mpango ovu wa dunia ya juu kutaka kuitawala Afrika umeegemea sana kwenye kudumaza na mwisho kuwatowesha wanaume wenye uwezo na nguvu ile ya asili.
Ni vile tu, tumeuingia mfumo bila silaha za kutosha kupambana wala mavazi ya kujikinga. Kuna wakati hua najiuliza, hivi ni kweli elimu huondoa ujinga? Kama ni kweli, mbona baadhi ya wasomi ndo chanzo cha ujinga? Mbona wale waliotembelea mataifa mengi duniani, hurejea na ulimbukeni? Mbona wenye uzoefu hutoa hamasa za kudumaza fikra na mawazo ya wale waliochagua kuwaamini?
Kiukweli, nahitaji sana pesa. Nataka nitembelee wanawake, nikianzia Pwani ambako ukatili unaanza na mwanamke mwenyewe kuuchochea, nitaishia Bara ambapo kukatiliwa kwa mwanamke kumemgeuza kuwa katili mwenye vyeti. Nitawaambia hili kwa hisia sana. Chini ya jua hili, sote tunategemeana. Tukishindwa kufaana kimapenzi tufaane ki maamuzi. Kama ndoa imeshindikanika kabisa, kama ulipata mtoto bila makubaliano na babaye, kama mwenza mwanamume amefariki, kama ni mtalaka na una watoto, kaa chini tafakari sana, jiruhusu kuyasikia maumivu wakati huo ukitafuta msaada ili upone.
Mlee mtoto kwenye misingi ya kuthamini na kuipenda jinsia yake. Haijalishi baba yake alikutendea nini, mtoto haimuhusu. Anahitaji malezi kutoka pande zote mbili. Kama ni ngumu mno ama imeshindikana kabisa, basi hakikisha kuna mtu mwenye jinsia ya kiume ambaye anaweza kukushika mkono katika malezi. Ama ni nduguyo au kiongozi wa dini. Mkumbushe mwanao mara zote kuwa hakuumbwa vile alivyo kimakosa.
Niliandika siku moja, watoto wa kiume hujifunza kwa baba zao jinsi ya kuwa wanaume na watoto wa kike hupewa ujasiri na baba zao. Ikiwa wewe ni mwanaume na kwa dhamira ya dhati unatelekeza watoto, tambua tu, unaandaa kizazi cha aibu na kesho ya uchungu kwako na kwa watu wengine wenye hofu ya Mungu.
Zipo sababu nyingi za huu uotofu unaoendelea chini ya hili jua. Nilisikia kuhusu vyakula na madawa yanayotoka hukooo mbali kuja kulegeza nyonga na kuchochea homon za kike kwa watoto wa kiume, (sina uhakika na hili) nimesikia kuhusu waganga chochezi wanaotuma ndugu kulawiti ili kufanikiwa kiuchumi. Nimesikia juu ya mengi ambayo yanahusisha moja kwa moja maisha ya watoto wetu, mashuleni, mahospitali, baadhi ya nyumba za ibada na hata majumbani.
Nikipata hela basi ziara yangu itakwenda moja kwa moja kuongea na watoto walio kwenye umri wa kuelewa na ningewaambia juu ya dalili hatarishi kabla ya ukatili ambazo kama watazisema mapema zitakuwa kinga kwao. Watapata msaada kabla ya dhahma. Nitawaambia mwenye uwezo wa kuuchukua uhai ni Mungu tu, hivyo wasiogope kuutetea utu wao kwa kusema ukweli pindi wanapojikuta kwenye hali tete ya kukatiliwa.
Sintoishia kwa watoto tu, nitasogea na kwa vijana. Baadhi yao huupitia ukatili kwa kuridhia wenyewe. Hapa naongelea ushawishi wa marafiki na tamaa za mafanikio ya haraka. Kwenye miji iliyokuchwa, vijana wa hovyo akili zao ni kupata jimama walikomoe, mabinti ni kupata mume wa mtu wamchune. Wasichoelewa ni kwamba kuzoea kujipatia riziki/kipato kwa njia ya mkato ni kama urahibu wa madawa ya kulevya, ukikosa vya kubwia utanunua hata vya kuvuta. Siku majimama yakiahirisha kukomolewa nini kitatokea? Siku wame za watu wakiahirisha kuchunwa ni nini kitatokea? Zipo njia nyingi za kujipatia kipato zisizoathiri hata nukta ya utu wako.
Kama binadamu umeumbwa na uwezo fulani ndani yako wa kufanya mabadiliko japo madogo hapa duniani. Uvivu unaua sana uwezo wa kufikiri. Kupenda mteremko kunalaza ubongo na kukuletea hasara yenye majuto mengi uzeeni. Wakati wa ujana ni wakati wa mapinduzi, mageuzi na kuchukua hatua zenye uthubutu wa makusudi.
Nikupe kisa kidogo nilichosimuliwa na mhanga wa tamaa yake mwenyewe.
Kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 25, alijikuta akigeuzwa 'mkorosho' kwa tamaa ya kupata dollar mia tano kwa usiku mmoja, ni yapi matokeo yake basi? Bandu bandu humaliza gogo' baada ya kukolewa na pesa alizoona anazipata kirahisi, alibadilika na kuwa rasmi mfanyabiashara wa utu wake. Ndani ya mwaka mmoja alitopea na kujikuta kwenye njia isiyo na namna ya kurudi nyuma.
Tunapata kuona namna msingi usipokuwa imara nyumba huanguka. Msingi wa mtoto yoyote upo mikononi mwa hekima ya mzazi. Hekima ya mzazi ipo kwenye kumcha Mungu na kuyadumisha mapenzi yake.
Kuna lugha nyingi sana za kuongelea jambo lenye kuumiza na kukatisha tamaa bila kuonyesha dalili za kulihalalisha. Kuna namna ya kunyoosha maelezo na misimamo bila kukatili hisia. Kuna kitabu nilisoma jina limeniponyoka ila mwandishi aliandika hivi, "Kama mcha Mungu atampenda mdhambi na kumkumbatia iko namna anaweza kumshawishi kubadilika. Lakini kama mcha Mungu atamtenga na kumnyanyapaa mdhambi ana nafasi kubwa ya kuwa amechangia uundwaji wa kishawishi wa wadhambi wengine mfano wa yule aliye tengwa"
Hii haimaanishi ukutanapo na watu wenye haiba zisizoelezeka vizuri kwa uwazi uanze kupiga nao picha, uanze kutoka nao mitoko yao, uanze kuingia kwenye vikundi vyao, hapana. Jichukulie wewe mwenye maarifa kama mbegu, popote uwapo hakikisha una mea. Usipotumia akili uangukapo topeni, utaishia kujichafua kwa mikono yako mwenyewe. Bila shaka umeona baadhi ya watu maarufu walivyojikuta hatarini kupoteza sifa zao kwenye jamii baada ya kuwa na urafiki wa karibu na mashoga. Kuna vijana huko mbali walijiaminisha wako kwenye njia sahihi baada ya kuona watu wa aina yao wana mahusiano na watu wazito. Ni hivi chunvi ikiharibika hakuna cha kuitia iwe sawa, kama wewe ni chunvi, kubaki kwenye njia sahihi na kufanya mambo kwa usahihi kutakusaidia kuponya na sio kuishia kuwa mgonjwa.
Tunatofautiana nguvu, kuna jambo utalifanya kwa nia njema ya kutangaza uwepo wake kwa jamii ukaishia kuwavutia watu dhaifu. Chunguza na chunga sana habari unazosambaza katika mitandao yako. Chunga mno kuelezea njia za kufanikiwa kwako kama zilihusisha kuuza utu wako. Kuna njia mbaya ulipita ukafanikiwa na ukaishia kuwa shujaa nikipita mimi nitazama na kuishia kusahaulika. Habari zina sambaa sana zama hizi, hakikisha huwi chanzo cha habari itakayopotosha na kuharibu kabisa maisha ya wengine.
NIKIPATA NYENZO ZA KUNISAIDIA, NITAELIMISHA BILA KUCHOKA.
Ni mimi wako katika ujenzi wa taifa, . Kungwi wa kisasa.
0742 6301 41
Hifadhi namba yangu niambie nihifadhi yako, tusafiri pamoja. Karibu vitabu vyangu vya maarifa kwa mwanamke. Asante.