Nahitaji shamba la kununua kwa ajili ya kilimo na ufugaji

Nahitaji shamba la kununua kwa ajili ya kilimo na ufugaji

DALA

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2009
Posts
2,256
Reaction score
4,647
Habari mabibi na mabwana?

Naomba mwenye kujua yanapopatikana mashamba ya bei nafuu, mashamba yanayofaa kwa shughuli za kilimo na ufugaji anifahamishe.

Ningependa kufahamu bei kwa ekari na ukubwa. Mimi ni mjasiriamali mdogo hivyo mtaji wangu pia siyo kubwa kihivyo.

Naomba kusaidiwa.
 
Mkoa gani unapendelea, na nia aina gani ya kilimo unataka kufanya? Na walau bajeti yako kwa ekari umetenga kiasi gani ili pia tuweze kukushauri
 
Mimi ninalo mwasonga nauza 7m kwa heka...
Weka budget yako
 
ungetaja mkoa aina ya zao na bajeti yako kwa hekari..... kuna mashamba used hayo usipowekeza pesabutalia...,. usipende vya bei nafuu
 
Mkoa gani unapendelea, na nia aina gani ya kilimo unataka kufanya? Na walau bajeti yako kwa ekari umetenga kiasi gani ili pia tuweze kukushauri
Maswali kibao,kama una shamba taja location na bei yako, acha usumbufu
 
Maswali kibao,kama una shamba taja location na bei yako, acha usumbufu
Wewe nawe mbona unakuwa kama sio kilaza? Mtu anakwambia anataka shamba, hajasema budget au location. Utamuelewa? Mtu akija kukwambia anataka nyumba, lazima utamuuliza budget na location. Usitumie makalio kufikiri
 
Nina shamba kubwa hela 90 ziko Njombe. Km 30 kutoka Njombe mjini.
Nilipanda miti ya mbao pain mwaka 2012,miaka 6 baadae ukapita moto. Ikabaki miti kiasi. Kwa sasa ni miti mikubwa.

Shamba lina mito isiyokauka kila upande. Yaani upande wa magharibi umepita mti na upande wa mashariki umepita mto.
Linafaa kwa kila aina ya kilimo iwe mahindi,uwekezaji wa muda mrefu,miti ya mbao, parachichi na pashen.

Nitakuuzia milioni 40 tu pamoja na miti iliyomo.
 
Njoo umalila ,heka ni sabuni kukodi ,Ila jifunze kunywa ulanzi ili uendane na wakazi sio tuanze kuhisi snitch umekuja kutuchora
 
Back
Top Bottom