Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 893
- 1,021
NAMTAKA SINGO MAZA
1 Nimehangaika sana, kuyatafuta mapenzi
Niliowapa amana, hata hawakuienzi
Nikapigwa dana dana, na kufanyiwa ushenzi
Namtaka singo maza, ndie nitayemuoa
2 Aloumizwa ja mimi, huenda tukalandana
Hatusikizi akwami, wawili tukipendana
Tukuze wetu uchumi, mawazo kuliwazana
Namtaka singo maza, ndie nitayemuoa
3 Kapita mingi mishale, hataogopa umande
Ajua haya na yale, kwa juhudi ajipinde
Mjuzi mambo ya kale, kucheza ngoma sikinde
Namtaka singo maza, ndie nitayemuoa
4 Asiwe mwingi wa wana, hapo hapatanifaa
Ukimwona kama mwana, hutadhani kashazaa
Awe mmoja wa ujana, ndoa tutaiandaa
Namtaka singo maza, ndie nitayemuoa
✍️Abuuabdillah
Whatsapp 0744883353
Kilimanjaro
1 Nimehangaika sana, kuyatafuta mapenzi
Niliowapa amana, hata hawakuienzi
Nikapigwa dana dana, na kufanyiwa ushenzi
Namtaka singo maza, ndie nitayemuoa
2 Aloumizwa ja mimi, huenda tukalandana
Hatusikizi akwami, wawili tukipendana
Tukuze wetu uchumi, mawazo kuliwazana
Namtaka singo maza, ndie nitayemuoa
3 Kapita mingi mishale, hataogopa umande
Ajua haya na yale, kwa juhudi ajipinde
Mjuzi mambo ya kale, kucheza ngoma sikinde
Namtaka singo maza, ndie nitayemuoa
4 Asiwe mwingi wa wana, hapo hapatanifaa
Ukimwona kama mwana, hutadhani kashazaa
Awe mmoja wa ujana, ndoa tutaiandaa
Namtaka singo maza, ndie nitayemuoa
✍️Abuuabdillah
Whatsapp 0744883353
Kilimanjaro