Wakiweka nitachukua, tuelekezane namna ya kusali.
Lamomy huna?
Sikuwepo jirani
Ngoja nimpe hii hapa 👇
NOVENA YA BIKIRA MARIA MFUNGUA MAFUNDO
Sala ya utangulizi:-
👉🏽Nasadiki
👉🏽Sala ya Imani
👉🏽Sala ya Matumaini
👉🏽Sala ya Mapendo
👉🏽Sala ya Katibu
👉🏽Sala kwa Maria Mfungua Mafundo
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Mama yetu mpole Maria mfungua mafundo, chanzo cha amani na Furaha, unayajua maisha yangu vizuri kwamba yamejaa mafundo ambayo yananifanya nikose hewa mara kwa mara. Yamenifanya mfungua na hivi ninaomba ukombozi kutoka kwako mama. Ninaaminia upendo wako wa kimama na ninajua kwamba kwa njia ya maombezi yako kwa mwanao, utayafungua moja baada ya jingine. Nataka kuishi maisha mapya ya mtoto wa Mungu a ninaamini kwamba bwana hataniacha bali atanipa maisha mapya ya mwili, akili na roho.
Naomba nisiwe peke yangu katika vita hivi vya rohoni, bali unielekeze na uniongoze ktk bonde hili la machozi. Pamoja nawe kama msafiri mwandamana ninauhakika wa kuwa kwenye njia sahihi.
Fungua Mafundo yangu yote leo ninaposubiri muda ule ambamo utafungua fundo la mwisho la maisha yangu nitakapokuwa huru mbali na dhambi zote na ninapomwona Bwana wetu uso kwa uso katika heri ya milele Mbinguni
Amina
🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Sala mafungu matatu ya Rozari
(Mafungu ya siku husika)
MAFUMBO YA FURAHA - Jumatatu
1⃣Malaika anampasha Habari Maria kwamba atakuwa Mama wa Mungu
2⃣Maria anakwenda kumtegemea Elizabeti
3⃣Yesu anatoka Hekaluni
Somo la Biblia
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Siku ya tatu kulikuwa na harusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwako. Yesu naye alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia"hawana divai"Yesu akamwambia,"mama nina nini nawe? Saa yangu haijawadia.Mama yake akamwambia watumishi"Lolote atakalowambia,fanyeni"
(Yohana 2:1-5)
Nakimbilia ulinzi wako Ee Maria Mama yangu. Kwa huruma na upendo wako na kujali kwako tayari unaona magumu yanayopitia familia yangu. Unaona machozi mchana na usiku.Unaona mapambano yanayoonekana kuendelea bila mwisho. Lakini kama unavyoiombea pia na kusema" Lolote atakalowambia fanyeni". Iombee familia hii ambayo imechanwa chanwa. vipande kwa umasikini ulevi matatizo ya kimahusia o maombolezo upotevu na ukame wa Kiroho.Nao.ba ifungue milango yake wazi ili Kristo aingie.Ili hili lifanyike,ninaweka katika mikono yako ya kimama fundo
.........
(taja fundo)
Najua utalifungua na Kristo atachukua mahali pake stahiki katika familia hii.Sikiliza sala yangu Maria na uwe kielelezo changu na kiongozi wetu
Maria mfungua mafundo, niombee mimi ninayekukimbilia
Sali mafungu mawili ya mwisho ya Rosali
4⃣Yesu anatolewa Hekaluni
5⃣Maria na Yusufu wanamkuta Yesu Hekaluni
SALA YA MWISHO
Bikira Maria mfungua mafundo
Maria mama yetu mfungua mafundo kumbuka kwamba haijasikika kamwe kuwa aliyekukimbilia akitaka umsaidie ulimwacha bila kusaidiwa. Nikichochewa na matumaini hayo na nikielemewa na dhambi zangu na mateso yangu ninakimbilia ulinzi wako kwa moyo wa majuto Ee mama. Mama wa Neno la Mungu usiakatae maombi yangu lakini unihurumie na usikilize Sala yangu.
Unafungua mafundo yote katika maisha yetu Ule mkanda mrefu wa mafundo unanyooshwa katika mikono yako ya kimama na ya Mapendo Sasa nakuja kwako Ee Bikira wa mabikira, ona mafundo mangapi yananiziba pumzi maisha yangu. Unao mateso ya maisha tena na tena.
Unaona nilivyopooza.Ee Maria uliyepata neema Imakulata mwenye kufungua mafundo katika maisha ya wanao naweka mikononi mwako marinda haya
👉🏽Changamoto za Kiroho
👉🏽Changamoto mahali ninapofanyia kazi
👉🏽Changamoto ninazozibeba katika maisha yangu na ambazo hazina ufumbuzi
👉🏽Mafundo yaliyosababishwa na tabia yangu, kukosa uvumilivu kukosa uwezo wa kuisikiliza, hasira, wivu, kutaka kulipa kisasi mashindano woga, chuki, kukosa usalama, kiburi, kutovutiwa na wenzake, hangaiko la moyo huzuni, urafi kushindwa, na uchoyo.
👉🏽Mafundo ya mioyo yetu iliyo migumu inayotuzuia kupenda kwa ukarimu na kusamehe kwa unahisi
👉🏽Mafundo yanayosabaishwa na matambiko,mazingaombwe, ushirika, uchawi, kupiga ramli.
👉🏽Mafundo kama matokeo ya kutoelewana katika familia Kati ya wazazi na watoto
👉🏽Mafundo ya kukosa ajira
👉🏽Mafundo ya msongo wa moyo kati ya mme na mke
👉🏽Mafundo yatokanayo na ulevi wa kupindukia na matumizi ya madawa ya kulevya
👉🏽Mafundo ya matokeo ya ugonjwa usiotibika
👉🏽Mafundo yanayosababishwa na maumivu Kutoka kwa wengine
👉🏽Mafundo yanayosababishwa na kuhukumiwa na dhamiri na utoaji wa Mimba.
Kwa unyenyekevu na kwa UTUKUFU wa Mungu tunakuomba ufungue mafundo haya yasiwepo tena milele.
Tunakutumainia kwa kuwa wewe ni faraja yetu pekee Ee mama. Yapeleke yote kwa Yesu mwanao Bwana wetu. Kwa maombezi yako yenye nguvu hakuna fundo hata moja linaloweza kubaki limefungwa.Kwa Imani kubwa tunatamani ulinzi wako wa pekee na wa uhakika maana hakuna aliyekimbilia msaada wako akakataliwa.Maria mfungua mafundo utuombee kwa Mwanao na Bwana wetu sasa na hata milele.
Amina.