Mwelewa
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 2,343
- 3,284
Uliumwa kwa muda mrefu right? Hapa nadhani stress zako zinatokana na ugonjwa uliopitia. Je familia ilikutenga wakati ukiugua? Marafiki shuleni waliwazia vibaya kuhusu ugonjwa wako hadi ukahisi aibu sana kuugua ugonjwa huo? Mimi nakuelewa unavyosema inatokea tu unakuwa na mambo mengi unayawaza kichwani na hiyo hali inakunyima uhuru/furaha. Ni kama vile unashindwa udhibiti lipi na uache lipi katika hayo mambo mengi unayowaza. Nakushauri ukijisikia hali kama hii jitahidi uyaruhusu hayo mawazo mengi yatiririke kadiri yatakavyo? Je utaweza kufanya hivyo? Pia kataa hali yoyote inayokujia kama vile kuchanganyikiwa coz watu wengi wenye hali kama yako hudhania wanaenda kuchanganyikiwa. Na hapa hali huwa mbaya zaidi. Hali yako ikizidi kuwa mbaya usione hatari kuvisit hospital. Mkuu usiogope hiyo hali itaisha vijana wengi inawatokea.....wengine hawaelewi hata ni nini. Yes I.