Nahitaji ushauri wa biashara, nina mtaji wa 1.2(million moja na laki mbili)

Labda atlist uongeze 1.2 +1.2 uwe na 2.4 atlist ..
Maana kwa 1.2 haitatosha, itakulazimu ununue bidhaa chache kutokana na mtaji wako,

mauzo yatakuwa kidogo kwasababu bidhaa nyingi utakuea hauna..

Mzunguko wa pesa wa biashara yako utakuwa mgumu siku za mwanzoni.. hadi kuzoeleka .

Ita idi uwe na akiba kidogo usije ukaitumia faida au kupunguza mtaji kwa matumizi binafsi..

Ushauri : fungua biashara ndogo itakayoendana na mtaji wako..

Kisha ukikuwa ndipo utimize malengo yako ya duka la mahitaji ya nyumbani..!

maana 1.2mil kama huo mtaa utakaofungua duka kuna ushindani , basi wewe unakuwa kwenye nafasi ya kushindwa zaidi..

Zingatia biashara ambayo gharama za uendeshaji ziwe ndogo na himilivu.. usije ukajiingiza kwenye makodi ya fremu / umeme wa kuchanga utata hadi 15+/month
Makodi ya serikali kwa pesahiyo hiyo!!
 
Biashara zipo nyingi ndugu kuna, biashara ya viungo Kama Hiliki karafuu n.k inategemea interesting yako lakini njia za kupita zipo
 
Mleta mada natumae ulipata muongozo...
 
Mkuu duka la reja reja linalipa sana, tafuta location Kawe pale, ile mitaa karibu na uuwanja wa Pakers (Kwa mwamposa) pale kuna movement sana, Chagua bidhaa zako chache na uzisimamie kwa bidii au hata popcorn tu zile siku za ibada yule Mchungaji anajaza sana watu pale lazima uuze..

Choose wisely vitu unavyotaka kuanza navyo.
Thanks.
 
Ulishawahi fanya hiyo biashara ya kufungua kiduka hapo awali?
 
Mkuu Jiulize kwanza hiyo milioni 1.2 uliipataje? Kama uliipata kwa kufanya shughuli furani bas mkuu usiiache hiyo shghur just unachotakiwa kufanya ni kuongeza value katika hiyo shughur iliyokuletea hiyo milioni 1.2, usiingie kweny biashara mpya hiyo pesa bado ni ndogo
 
Shukran sana kwa ushauri
 
Unapenda biashara ya duka je umewahi kufanya biashara yoyote hapo kabla?
 
Ok, iyo ya duka inaweza ikakomba hela yote uliyonayo maana lazima upange fremu

Nilitaka kukuambia uwekeze nusu ya pesa uliyonayo wakati nusu ingine umeiweka Kama akiba ukiwa unasikilizia maendeleo ya biashara lakini kwa biashara ya duka sidhani Kama itawezekana.

Mwanzo ni mgumu na biashara yoyote changamoto hazizuiliki hiyo pesa ni nyingi sana na ni ndogo sana inategemea na wewe ulivyojipanga hata kwenye ajira wanataka mtu mwenye uzoefu na kwenye biashara ni hivyo hivyo?

Utapataje uzoefu?

Wekeza hiyo laki mbili hiyo milioni ifiche
Fanya utafiti tafuta biashara ya laki au laki mbili fanya baada ya muda utakuwa umepata uzoefu mkubwa sana na hiyo milioni itakusaidia mbele ya safari.

Narudia tena usiweke mayai yote kwenye kapu moja.
 
Shukran kwa ushauri
 
Hapa labda anunue kitu kinoma kimoja. Mfano sukari mfuko mmoja, mchele labda kilo mia, mafuta ya kupikia ni deal sana maana nimeuza ila faida yake i nahitaji uwe na roho ngumu sana.
 
Anzisha danguro...inalipa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…