Nahitaji ushauri wa haraka sana maana nahisi Nachanganyikiwa sasa

Nahitaji ushauri wa haraka sana maana nahisi Nachanganyikiwa sasa

Pole sana kiongozi, inshort huyo mwanamke wala hakubakwa alitoa tu mwenyewe kwasababu ya upweke alionao,wanawake wengi ni wazaifu hasa wanapokuwa kwenye hali kama hiyo,inawezekana huyo jamaa alikuwa anamtongoza sana au amempenda tu na akiangalia wewe uko mbali,mwili unataka huduma lazima ashawishike tu,chakufanya mchukue uwe nae karibu,endelelea kumsoma nyendo zake kama ukiona wanaendelea kuwasiliana basi fanya maamuzi magumu tu.
 
Msamehe tu. Ukiangalia umri umeenda. Hata watoto wenu watakua wakubwq sasa. Uzuri hakubishq amekwambia ukweli japo kwa njia nyingine. Naimani hatorudia tena na anajutia.
By the way unaweza nifundisha jinsi ya kufanya hivyo meditation Nina shemeji yako hapa kisu atari Nina wivu naye kinoma nataka nim monite.
 
Mkuu pole sana. Ila usimuache mkeo. Hata kama amekusaliti kwa makusudi sio kwa kubakwa na huenda hata sasa anaendelea kupigwa na microfinance guy ila usimfumkuze kwa haraka. Ioe situation muda angalau hata mwezi to miezi mi 3 na katika kipind hiki muwekee msimamo wako kabisaa kuwa huwez kuwa nae ila msimuache. Ataizoea hali ua msimamo wako na wewe utatumia kipind hiko kuweka mipango hasa utaratibu kuhusu watoto then mkatae mazima
 
Ruge Mwongaza Njia Alifariki Na Miaka 48 Na Watu Waliimba Na Kusherehekea Maisha Yake
Wakisema Amefariki Akiwa Kijana Mdogo Sana

KKwahiyo 46 Bado Sana

Ushauri Wangu Ishi Na Mkeo Hata Ukimwacha Utaoa Na Utazaa Tena, Wale Watoto Wako Watapata Tabu
Duh mapenzi.
Ruge 46
Nandi 30

Differrence 16.
 
You own nothing and nothing should owns you detach from everything move on mkuu.
 
Habari wanajamvi naandika Bango Hili nikiwa sijui nini nifanye na nikiwa nimechanganyikiwa Kwa Yaliyotokea na sielewi hili.wala lile.

IKo hivi Mimi ni Kijana mwenye Umri wa Miaka 46, Nilikuwa nina Mke wangu ana Umri wa Miaka 34 Tulikuwa Tunaishi naye lakini kutokana na mambo Ya kimajukumu Ukabidi Niende Dodoma kama miezi mitano au sita Ilopita Na yeye Nikamuacha Tabora.

Tulikuwa tunawasiliana Vizuri tu na kuna kipindi Ilitokea Shida kidogo mwezi mmoja baada ya mimi Kuondoka, Kulitokea Hitilafu Kwenye Ujenzi tunaofanya hapo Kahama kwakuwa nilikuwa mbali na yeye Ni mfanyakazi wa Serkali nikamuomba akakope Pesa Kiasi halafu nitakuja Kufidishia (Ndiyo Tinavyofanya siku zote).

Kama Jukumu likiwa la kwangu na yeye akiwa na means ya kufanya bhasi anafanya Mimi naandika deni.

Kwakuwa Benki walikuwa wanachelewa Ikabidi aende kwa wanaoacha Kadi akafanikiwa na kupata pesa na kila mwezi akawa anakatwa pesa zake na alikuwa anafata kiasi kinachobaki hapo ofisini..

Wiki Moja kabla nikawa Nahisi Kama Kuna uwezekano Mke wanhu ananisaliti (Mimi ni mtu wa Kufanya Sana Meditation Hivyo Hisia zikinijia bhasi lazma nizifanyie Meditation Kwa siku angalau mbili na huwa napewa clear Picture)..

Kipindi nafanya Meditation nikawa naona kabisa Mke wangu ananisaliti sasa Baada ya miezi minne kuondoka huko Nikawa namuuliza Huko ni salama mbona kama kuna kitu kibaya unafanya jibu lake hakuna shida yoyote.

Guyz huyo jamaa wa Microfinace simjui na Sijakutana naye ila kuna kitu kikawa kina niambia nimuulize Wife na nimkazanie kuhusu Huyo mtu kwa nguvu mpaka aseme ikibidi Nitumie uongo wowote kama mwanaume..

Nilifanikiwa Kimlazimisha na kumuuliza hatimaye akaamua kugunguka kuwa yule Jamaa wa Microfinace alimbaka Yeye alipokuwa Ofisini kwake Kuchukua Kiasi cha Pesa Kilichobaki na wala haikuwa dhamiri yake.

Nikamuiliza Umereport tukio hilo akajibu "Hapana"
Nikamuuliza Ulipiga kelele akajibu "Hapana maana nisingesikika wala watu wasingeniamini"

Nikawaza sana huyu Wife nimezaa Naye watoto watatu..
Na anassma alimbaka Miezi minne Exactly tangu nilivyoondka ila nisingemuuliza Nadhani ingeendelea Kuwa story ya siri yake..

Ninawaza kumpa Talaka Tatu ila bado nahofu na watoto wangu Nimempa Talaka 2 ila akili yangu bado inaona nimeumizwa sana nastahili kufanya kitu ila bado moyo unavuja damu nifanye nini??

Naombeni wan JF mnishauri Nifanye Nini maana naumia Sana.

Na kwa maelezo yake Bado siamini kabisa.

Naombeni sana Ushauri maana ametishia Kujiua endapo sitamrejea
Tumia hiyohiyo meditation ikupe ushauri km ilivyofanya kukuonyesha maovu ya usaliti wa mke wako usitusumbue sis wenyew tunastress zetu
 
Back
Top Bottom