Nahitaji ushauri wako kuhusu saratani ya damu

Satuuuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2015
Posts
1,849
Reaction score
1,993
Wapendwa habari zenu,

Tatizo lenyewe ni kuwa katika hali ya kupambana na Cancer ya Damu, ilikua 2014 mwanzoni nilipoanza kuhisi uvimbe tumboni ndipo nilipoamua kwenda Hospitali na kufanya vipimo ambapo kwakweli majibu yalionyesha tu kuna uvimbe wa bandama na nilipewa tu vidonge vyakupunguza uvimbe.

Pia niliambiwa ukiendelea kuwepo basi watanipasua na kuitoa bandama jambo lililonipa wasiwasi sana, siku zikazidi kwenda uvimbe unaongezeka nilipofika hospitali nikaongezewa doze, baada ya kuanza kutumia vidonge na doze ikiwa imeongezwa afya ikaanza kudhoofika ndipo nilipo amua kuvuka mpaka na kwenda nchi ya jirani walipo gundua kuwa nina tatizo la Cancer ya Damu.Nikaanzishwa dawa ya kuua makali na cells za cancer ambazo bado naendelea kuzitumia.

Ombi langu kwenu wapendwa najua katika wingi wetu humu JF wapo watu wenye kujua zaidi juu ya tiba mbadala ambazo nimesikia kuwa zipo Ila kwakweli sizifahamu, pili niliwahiambiwa kuwa Serikali husaidia matibabu ya Cancer kupitia kuchangia gharama au kutoa dawa lakini kwangu binafsi sijui wapi pakuanzia.

Nimekuja kwenu naitaji ushauri kutoka kwenu.
 
Kuna baadhi ya Kansa za damu zinatibika hata kama umechelewa kuanza matibabu, nenda pale Ocean road hospital kuna madaktari bingwa wengi tu wa magonjwa ya kansa, sema kama huna insurance na huna uwezo kifedha huwezi kumudu gharama za matibabu kwa sababu madawa yake ni gharama kubwa sana hapa tunazungumzia mamilioni ya hela
 
Sawa,nikweli matibabu yake ni gharama sana , kuna nchi zinazotoa msaada wa dawa kwa wananchi wake mfano mzuri ni Kenya je hapa Tz mfumo huo pia upo ?
 
Pole ndugu! Madaktari wakp wanasemaje? Kama hujawahi kwenda, basi nenda Ocean road hospital, wanashughuloka na saratani tu pengine watakuwa na kitengo cha utafiti na kuweza kukusaidia.
 
Mungu atafanya njia mkuu, mtumaini yeye atakutetea!!
 
Pole sana kaka na nadhani take advantage ya hizi Bima za Afya kama NHIF. Kuna mtu aliniambia kua ukijiunga na Mfuko wa PSPF then wanakuunganisha na Bima ya NHIF na hapo unaweza kutibiwa katika Hospitali with no cost.
 
Naomba kujua unakaa wapi?

Weka namba yako ya simu hapa nitakupigia.
 
Pole sana kaka.
Cha kwanza kabla ya matibabu yote ya mwili mwamini Mungu kuwa anaweza yote . Pili uponyaji huendana na stability ya roho akili na mwili wako. Hivyo kwa imani yako yoyote zidi kufanya ibada. Pia amini kuwa you are stronger that the disease. Tatu anza sass lifestyle inayoenda kupunguza makali ya magonjwa yote. Acha matumizi ya processed foods , acha matumizi ya excess starch na sugar. Jikite kwenye gree foods , lots of water and oxygen .
Tatu: Do all the readings you can about that disease. Hata kama unaenda kwa wataalamu kama upo kwenye nafasi ya kuresearch itakupa mwanga hata wa kujadiliana na daktari kuhusu treatment plan anayosuggest kwako. By reading other related success stories utajua the DOs and DONTs. Soma pia kuhusu alternate cancer treatments ( use of laetrile, wheat grass, blackstrap mollases etc) . In all these omba Mungu akuongoze kwenye right plan and trust your choice.
Unapokuws mgonjwa utapata ushauri mwingi sana ila kama una all the needed information inasaidia kumake the right choises.
God bless you and We trust and pray you rise up as a Hero.
 
Pole mkuu ,
Mungu akutangulia na njia za upoji zifunguke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…