Nahitaji ushauri wako kuhusu saratani ya damu

Kina kitu kinaitwa trevo japo sina uhakika nacho lakini wengi wanatoa shuhuda kuwa inasaidia cancer, jaribu ndugu yangu. pole sana.
 

POLE SANA KAKA,NAOMBA UNIJULISHE MAENEO GANI YA TUMBO YALIKUWA YAKIUMA?NATAKA NIFAHAMU PIA MANAKE KUNA KIPINDI NILIAMBIWA NINA MATATIZO YA BANDAMA NIKAENDA HOSPITAL KUPIMWA DOCTA AKANIAMBIA BANDAMA YANGU IPO VIZURI LAKINI SIJIELEWI ELEWI,HEBU NAOMBA UNIJUZE DALILI ZAKE MKUU.
 
Pole sana mkuu kama wadau walivoshauri nenda ocean road na reference ya matibabu ya mwanzo watakupokea, mapema ni bora zaidi.
 
Asante sana mkuu hakika nimepata mengi
 
Pole sana kaka na nadhani take advantage ya hizi Bima za Afya kama NHIF. Kuna mtu aliniambia kua ukijiunga na Mfuko wa PSPF then wanakuunganisha na Bima ya NHIF na hapo unaweza kutibiwa katika Hospitali with no cost.
I wil make a follow up
 
Pole mkuu nini ilikuwa indicator ya kujua kama ulikuwa na uvimbe tumboni???
Niliweza kuhisi kitu tofauti hasa nyakati za kulala ilikua naweza kuhisi kuna uzito flan na ugumu wa kitu upande wa kushoto
 
Kama hauna bima ya afya, jiunge kwanza bima ya afya hata kupitia PPF itakusaidia sana, kutibiwa kwa cash lazima utakufa masikini. Mungu akubariki.
 
Ni upande wa kushoto unaweza hisi uvimbe kwa kujigusa au maumivu kwa mbali
 
Ukiwa unaendelea na matibabu yako, kila mara ukipata muda, chukua kitunguu swaumu kitwange au kikuangue ( kama vile unataka kupikia labda mboga), kisha kiweke kwenye kikombe, kisha chukua asali kijiko kimoja weka ndani ya kikombe chenye kitunguu swaumu, harafu kata limao nusu kamulia ndani ya mchanganyiko wa hiyo asali na kitunguu swaumu. Baada ya hapo chemsha maji weka ndani ya kikombe hicho. Kunywa kama chai. Kila siku upatapo muda ( hakikisha kwa siku unakunywa si chini ya siku mbili). Utashangaaaa! ...... Jitahidi kutumia na usiache dawa zako endelea nazo
 
Nimesahau kitu.....unatakiwa kunywa huo mchanganyiko asubuhi kabla hujala kitu na vitunguu swaumu viwe vingi uwezavyo na uvimeze usiviache kwenye kikombe (kwa hiyo nivema unywe huku unakologa ile umeze vyote). Baada ya hapo mchana unaweza kunywa wakati wowote.... Ukitumia baada ya mwezi mmoja uje PM uniambie unaendeleje.......ni tiba usidharau tafadhari
 
Incase ukisikia nguvu zinaisha mwilini, utachemsha tangawizi (tangawizi iwe kali sio kama ile unayoweka kwenye chai ) kicha utaweka sukari kwa mbali, unywe baada ya saa moja ukimaliza kupata lunch.
N.B.. Tangawizi inyweke kama utasikia mwili unapoteza nguvu. ( ujilazimishe kula maana tangawizi itakupa nguvu nyingi na hautasikia hamu ya kula).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…