Nahitaji ushauri wako kuhusu saratani ya damu

Nahitaji ushauri wako kuhusu saratani ya damu

Agiza matunda yanaitwa mafyulisi(mbeya) au pingas(iringa) waingereza huita apricot. Nasikia yanasaidia sana mno. Ni vema ukaanza fasta. Kwa ushauri zaidi mtafute membermoja humu anaitwa Deception atakujuza zaidi
 
Mimi nazungumzia sayansi,wewe unaleta siasa.Sayansi na siasa ni mambo mawili yanayopingana.Endelea na siasa,mimi naendelea na sayansi....watu kama ninyi itawachukuwa muda sana mpaka kuamka...

Vipi wale wanaowahi kwenda India kwa matibabu ya cancer lakini hawaponi?Hao mbona huwazungumzii?
mm na ww anayeleta siasa ni nani? sayansi gani unayozungumzi ww au tiba mbadala nayo ni part of medicine or science-based healthcare systems? serikali ya marekani hutumia zaidi ya $2.5 billion kila mwaka kwa kulipa watu kutest tiba mbadala with almost none showing any effect beyond that of false treatment. Jobs alikufa kwa cancer inayotibika sababu ya kukataa matibabu na kuamini kuwa tiba mbadala itamsaidia nakusababisha unnecessarily early death
 
Agiza matunda yanaitwa mafyulisi(mbeya) au pingas(iringa) waingereza huita apricot. Nasikia yanasaidia sana mno. Ni vema ukaanza fasta. Kwa ushauri zaidi mtafute membermoja humu anaitwa Deception atakujuza zaidi
Nashukuru mkuu nitalifwatilia hilo ili nijue zaidi
 
Kama utakuwa na muda wa kuweza kuangalia video na kusoma emails, nitumie email address yako pm ili nikugorwardie email za centre moja ya matibabu ya cancer hapa USA. Kisha nita kulink ili uwe unapata email zao daily.

Kuhusu cancer, ni ugonjwa ambao ukifuatilia hawa scientists nitakao kupa utagundua yafuatayo.
1. Ni ugonjwa unaotibika kiurahisi
2. Madaktari hawajui lolote kuhusu cancer maana they are brainwashed
3. Ni ugonjwa ambao pharmaceutical companies wanautumia kupata pesa
4. Hata kipimo tu cha cancer ni source of cancer

Samahani siwezi weka email address yangu hapa sababu ya hackers
 
Wapendwa habari zenu,

Tatizo lenyewe ni kuwa katika hali ya kupambana na Cancer ya Damu, ilikua 2014 mwanzoni nilipoanza kuhisi uvimbe tumboni ndipo nilipoamua kwenda Hospitali na kufanya vipimo ambapo kwakweli majibu yalionyesha tu kuna uvimbe wa bandama na nilipewa tu vidonge vyakupunguza uvimbe.

Pia niliambiwa ukiendelea kuwepo basi watanipasua na kuitoa bandama jambo lililonipa wasiwasi sana, siku zikazidi kwenda uvimbe unaongezeka nilipofika hospitali nikaongezewa doze, baada ya kuanza kutumia vidonge na doze ikiwa imeongezwa afya ikaanza kudhoofika ndipo nilipo amua kuvuka mpaka na kwenda nchi ya jirani walipo gundua kuwa nina tatizo la Cancer ya Damu.Nikaanzishwa dawa ya kuua makali na cells za cancer ambazo bado naendelea kuzitumia.

Ombi langu kwenu wapendwa najua katika wingi wetu humu JF wapo watu wenye kujua zaidi juu ya tiba mbadala ambazo nimesikia kuwa zipo Ila kwakweli sizifahamu, pili niliwahiambiwa kuwa Serikali husaidia matibabu ya Cancer kupitia kuchangia gharama au kutoa dawa lakini kwangu binafsi sijui wapi pakuanzia.

Nimekuja kwenu naitaji ushauri kutoka kwenu.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
ukweli naujua ila siwez kukushauri i felt sad naomba kilamtu a google source of cancer ili ajue jins ya kuepuka tatizo maana baadh ya kansa hazina dawa na tuepuke usasa tukidhan ni ufahal sijui soseji baga piza magarita spain wine na nk we kula dona bamia tembele togwa mbege na nk utakua salama
Hizo baadhi ya cancer ambazo hazina sawa ni zipi mkuu? Mbona kama unaeneza hofu zaidi kwa wadau kuliko tumaini?
 
kuna mtaalamu mmoja yupo sehemu unaitwa nyumba ya mungu katika wilaya ya mwanga hapa moshi.huyu mzee amesaidia watu wengi sana hadi madaktari wenye saratani mbalimbali amewasaidia na wamepona!kiukweli huyu mzee ni bingwa na hana gharama kubwa ila masharti yake ya kukutibu usiwe umechomwa mionzi na kansa isiwe katika ya mwisho kabisa!kwa hapo anakutibu na unapona kabisa mimi nna ushuhuda wa dada yangu alipata ya ziwa mwaka 2000 alitibiwa hadi leo amepona kabisa.na ameshapeleka ndugu na jamaa wengi kwa huyo mzee na wamepona kabisa.dawa za hospitali hazitibu zaidi ya kukudhoofisha tu.tafuta muda nenda hapo nyumba ya mungu ulizia KOKOTO utapelekwa na gharama zake hata elf50 haifiki halafu uje ulete mrejesho hapa ukichekelea
Anapatikana wapi Kokoto, Kilimanjaro?
 
Kama unachosema ni kweli,basi nitafute nikupe ushauri utakaokuponya kabisa na uwe mmoja wa mashuhuda humu.....
Vinginevyo hao waliokwambia uende ukapige chemo au mionzi na wale wanaokutaka ufanye maombi watakuua....cancer haitibiwi kwa maombi au mionzi....kuna watu wamekariri kwenda India lakini hakuna hata mmoja aliyepina cancer kwa kwenda India lakini bado wanang'angania kwenda India....watu kama sisi tunapowaelimisha watu kuhusu mambo haya tunadharauliwa...

Sasa kama kweli unataka kupona,usidharau,njoo nikupe ushauri,ni bure kabisa,sihitaji pesa kutoka kwako,bali nahitaji kiti kimoja tu,kwamba urudi tena hapa kutoa ushuhuda ili wengine nao wanufaike kupiti kwako...

Mungu ametupa akili tuitumie kutatua matatizo....matatizo hayatatuliwi kwa maombi PEKEE kwa maana hata mimi kuja hapa kukupa ushauri inawezekana ni moja ya majibu ya Mungu kuhusu hayo maombi...usidharau.
Mkuu Deception nakupongeza kwa hekima, maarifa, ujuzi na kipawa ulichopewa kuwasaidia kwenye uhitaji hususan kwenye eneo la matibabu.
Naona katika post yako hapo juu umesema cancer haitibiwi kwa maombi. Umekataa suala la maombi lakini hapo chini umeji contradict tena kuwa huenda Mungu amejibu maombi yake kwa wewe kujitokeza kutoa msaada. Nimefurahi kwa kuji contradict kwako which proves that God still answer prayers.
Mkuu, mwanzo umesema Mungu ametupa maarifa lakini unakataa kuwa kansa haitibiwi kwa maombi. Biblia inatuthibitishia kuwa Mungu mwenyewe alitibu magonjwa mengi ya mwanadamu kansa pia ikiwemo.
Huwezi kumweka Mungu mbali kwenye eneo lolote la maisha ya binadamu. Wapo watu wameponywa hadi ukimwi kwa maombi. Mungu bado anabaki kuwa mponyaji wa kwanza na wa mwisho. Mwanadamu anatumiwa tu.
Maarifa yako uliyopewa na Mungu yasikufanye usahau ukuu wa Mungu.
To your surprise unaweza kumpata Ndugu Satuuuu ukampa dawa na ukashindwa kumponya ukashangaa anaponywa na Mungu kupitia maombi.
Anyway,Mungu akuongezee maarifa kila umkumbukapo na kumwabudu.
Nilitaka kukukumbusha hilo tu. Nilidhani umesahau
 
Pole sana mkuu ila kansa ya damu inatibika na kupona kabisa japo ni ghali,nnao ushahidi namfaham jamaa yangu nlisoma nae chuo mwaka wa pili akagundulika na kansa ya damu,ila akapelekwa marekani na kapona kabisaaaaa nakurejea kumaliza elimu yake. Hapo ni pesa tu chamsingi kama uwezo haupo unaweza kufundrise mtafute mtu kama Sam Maela wa itv anaweza kukuunganisha na Watz wenzio na ukasaidiwa,uckate tamaa mkuu hayo mambo yanafanyika na huyo jamaangu yupo usa sasa maana mzee wake yuko huko na familia,chukua hatua na ukirejea huku wapo watu tunachanga tu mbona harusi kibao tunatoa pesa
 
Pole sana mkuu ila kansa ya damu inatibika na kupona kabisa japo ni ghali,nnao ushahidi namfaham jamaa yangu nlisoma nae chuo mwaka wa pili akagundulika na kansa ya damu,ila akapelekwa marekani na kapona kabisaaaaa nakurejea kumaliza elimu yake. Hapo ni pesa tu chamsingi kama uwezo haupo unaweza kufundrise mtafute mtu kama Sam Maela wa itv anaweza kukuunganisha na Watz wenzio na ukasaidiwa,uckate tamaa mkuu hayo mambo yanafanyika na huyo jamaangu yupo usa sasa maana mzee wake yuko huko na familia,chukua hatua na ukirejea huku wapo watu tunachanga tu mbona harusi kibao tunatoa pesa
Mkuu Asante umenipa mwanga
 
Hii thread nimeiona late ila kama binadamu I have to be so concerned. Pole sana kaka, ninaposema pole sina maana tatizo lako ni kubwa kuliko Mungu, hapana. Nimejaribu kusoma comment za watu nimeona kuna mdau kakushauri kuhusu kitunguu swaumu, asali na limao hivi vitu vinauwezo mkubwa wa kufanya magic, ningependa kukushauri kwamba katika Asali jaribu kutafuta ile asali ambayo ni pure, haijachakachuliwa na pia kuna sukari nyingi mjini ambazo zinatengenezwa na sukari guru, hizi haziwezi kufanya kazi kama asali orijino. Katika kununua asali zingatia sana hilo mkuu ili kupata tiba sahihi.

Mungu ni mkubwa kuliko matatizo /magonjwa yanayotusumbua.
 
Pole sana kaka.
Cha kwanza kabla ya matibabu yote ya mwili mwamini Mungu kuwa anaweza yote . Pili uponyaji huendana na stability ya roho akili na mwili wako. Hivyo kwa imani yako yoyote zidi kufanya ibada. Pia amini kuwa you are stronger that the disease. Tatu anza sass lifestyle inayoenda kupunguza makali ya magonjwa yote. Acha matumizi ya processed foods , acha matumizi ya excess starch na sugar. Jikite kwenye gree foods , lots of water and oxygen .
Tatu: Do all the readings you can about that disease. Hata kama unaenda kwa wataalamu kama upo kwenye nafasi ya kuresearch itakupa mwanga hata wa kujadiliana na daktari kuhusu treatment plan anayosuggest kwako. By reading other related success stories utajua the DOs and DONTs. Soma pia kuhusu alternate cancer treatments ( use of laetrile, wheat grass, blackstrap mollases etc) . In all these omba Mungu akuongoze kwenye right plan and trust your choice.
Unapokuws mgonjwa utapata ushauri mwingi sana ila kama una all the needed information inasaidia kumake the right choises.
God bless you and We trust and pray you rise up as a Hero.
Very strong message, mkuu maneno yako yana busara mno! kwa huyu mgonjwa na wengine wote.
Mazingatio ni muhimu sana katika ushauri huu.
Muumba akuzidishie busara, aamin.
 
Mkuu pole sana na pia namwomba muumba akuponye, lakini nikupe tahadhari pia katika maelezo yako umegusia tiba mbadala mimi nakubali tiba mbadala ipo lakini angalia hiyo tiba unaipata kwa nani maana jamaa wa tiba mbadala kipindi hiki wako wengi mno lakini wengi ni wa kuongeza tatizo badala ya kuondoa,kuwa makini na hilo.
Nataraji pia utakuwa umesoma maelezo ya mkuu kinyau kwa mtazamo wangu kuna busara kubwa ndani yake, tafakari.
Mwisho nakuombea tena kwa muumba akuponye kwani yeye ndiye mfalme wa waponyaji.
 
Mabazazi wote wanaokufata pm hujawaona mpaka ukataka kumtunza mtoa mada?
Stunter labda hujamwelewa miss natafuta, binafsi nilivyomwelewa mimi anajaribu kumfariji mgonjwa kwamba ugonjwa wake wala si tatizo kuuuubwa kivile so apunguze ama aondoe kabisa stress na mambo yaende kama kawaida ndo maana anaingizia jokes fulani hivi ili mgonjwa aondoe stress.
 
Back
Top Bottom