Hivi wanaoshindwa katika migogoro ya ardhi kwenye suluhu inayo tolewa katika mabaraza ya ardhi ya kata,nao wanaruhusiwa kukata rufaa katika baraza la ardhi na nyumba la wilaya?,na je asipokata rufaa ndani ya siku 45 Sheria inasemaje Kwa huyo mtu?
Utatakiwa kufanya maombi ya kuongezewa muda wa kukata rufaa(notice of extension of time to appeal) na katika maombi hayo utaandika kuwa moja ya sababu ya kuchelewe kukata rufaa ni kuwa ulichelewa kupata hati ya hukumu kutoka mahakamani. Na hiyo inatosha kabisa kukubaliwa.
Kuna changamoto moto mkuu kwenye maelezo yako kesi za ardhi hazisikilizwi mahakama ya mwanzo bali migogoro ya ardhi huwa inaanza kwenye mabaraza ya ardhi ya kata ikitoka hapo inaenda mabaraza ya wilaya ,sasa je wewe kesi yako ilikuwa baraza la wilaya au?