Kuna jamaa yangu miaka miwili iliyopita alisajiri line yake ya kampuni moja hivi ya mawasiliano. Alipotuma hela kwa mtu ika display jina la kike ingawa number ni ile ile. Hali hii ilitaka kuleta mgogoro ndani ya familia yake, kwamba ameipata wapi? Ameshatembelea ofisi zao zaidi ya tano ndani ya miaka hii miwili, na kila mara akijaza form na kutoa kitambulisho cha kazi lakini mpaka sasa hakuna mabadiliko. Kila ofisi aliyokwenda ilibidi atoe Hadith ndefu na kuwapatia number za mwanzo kabisa alizofanya nazo mawasiliano na wakala aliposajiri, na vithibitisho vingine. Mara zote aliahidiwa marekebisho baada ya wiki moja, lakini hakuna kilichofanyika.
Anampango wa kuwashitaki wamlipe muda wanaompotezea kupanga foleni masaa kadhaa kwenye ofisi zao.