Nahitaji wakili nikawashtaki tigo mahakamani

Nahitaji wakili nikawashtaki tigo mahakamani

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
Mimi ni mteja wa tigo tangu inaitwa buzz mpaka ikaja mobitel na sasa ni tigo sijui itafuata nini,waliposema tusajili nilikua mtu wa mwanzo na tukaambiwa hatutasumbuliwa tena. Tumevumiliana kwenye ups n down zooote mara meseji haziendi,mara simu hazitoki , mara line imeblock wameiba hela sasa hivi wananitumia meseji kua namba yangu haijasajiliwa na niende nikasajili tena. Sasa form ya ushahidi kua nilisajiliwa ninayo nataka nikawashtaki ili iwe fundisho kwa utendaji wao mmbovu kwanza hawana shukrani. Kama kuna wakili anasoma hi post na anaweza kunisaidia kwa hili tafadhali ni inbox.
 
Mi nakushauri nenda mahakama iliyopo jengo la ubungo plaza sifahamu ghorofa ya ngapi lakin huwez kupotea kama utauliza pale nilishawahi kufuatilia jinsi mtu unavyoweza kushtaki kampuni ya simu kama itakufanyia makosa uliyoeleza hapo juu, tena ukishinda kesi utalipwa fidia kubwa tu.
 
Asante mkuu ntafanya hivyo nawasubiri wafunge hii line , NAHAMU NAO SANA WAS********! WAMEZOEA SASA TUKINYAMAZA WANAJUA WOTE MAMBULULA
 
Mkuu sijakupata vizuri kuhusu hiyo mahakama iliyopo Ubungo Plaza! Unaweza kutufafanulia hiyo mahakama inaitwaje na inafanyaje kazi? Na kuhusu kuingizwa kwa kesi mahakamani, je kama mdai (complainant) unakuwa na uchaguzi wa kupekela madai yako mahakama yeyote uitakayo wewe?
Mi nakushauri nenda mahakama iliyopo jengo la ubungo plaza sifahamu ghorofa ya ngapi lakin huwez kupotea kama utauliza pale nilishawahi kufuatilia jinsi mtu unavyoweza kushtaki kampuni ya simu kama itakufanyia makosa uliyoeleza hapo juu, tena ukishinda kesi utalipwa fidia kubwa tu.
 
Kuna jamaa yangu miaka miwili iliyopita alisajiri line yake ya kampuni moja hivi ya mawasiliano. Alipotuma hela kwa mtu ika display jina la kike ingawa number ni ile ile. Hali hii ilitaka kuleta mgogoro ndani ya familia yake, kwamba ameipata wapi? Ameshatembelea ofisi zao zaidi ya tano ndani ya miaka hii miwili, na kila mara akijaza form na kutoa kitambulisho cha kazi lakini mpaka sasa hakuna mabadiliko. Kila ofisi aliyokwenda ilibidi atoe Hadith ndefu na kuwapatia number za mwanzo kabisa alizofanya nazo mawasiliano na wakala aliposajiri, na vithibitisho vingine. Mara zote aliahidiwa marekebisho baada ya wiki moja, lakini hakuna kilichofanyika.

Anampango wa kuwashitaki wamlipe muda wanaompotezea kupanga foleni masaa kadhaa kwenye ofisi zao.
 
Back
Top Bottom