mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 901
- 1,742
Mimi ni mteja wa tigo tangu inaitwa buzz mpaka ikaja mobitel na sasa ni tigo sijui itafuata nini,waliposema tusajili nilikua mtu wa mwanzo na tukaambiwa hatutasumbuliwa tena. Tumevumiliana kwenye ups n down zooote mara meseji haziendi,mara simu hazitoki , mara line imeblock wameiba hela sasa hivi wananitumia meseji kua namba yangu haijasajiliwa na niende nikasajili tena. Sasa form ya ushahidi kua nilisajiliwa ninayo nataka nikawashtaki ili iwe fundisho kwa utendaji wao mmbovu kwanza hawana shukrani. Kama kuna wakili anasoma hi post na anaweza kunisaidia kwa hili tafadhali ni inbox.