Naibu Spika Dkt. Tulia: Jesca Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya Spika haina taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako

Ukiwa muongo unapaswa kuwa na kumbukumbu sana (Liars must have a good memory). Bibi Tulia anadaia hajapata barua kutoka Chadema inayoonesha kuwa wanawake 19 walioko bungeni, walifukuzwa uanachama. Anasema wangekua wamefukuzwa wasingepaswa kuwepo bungeni maana ni kinyume cha Katiba.

Sasa tumemsaidia kumkumbusha kwamba barua ilitumwa na ilipokelewa ofisi ya Spika tarehe 1/12/2020 tena kwa dispach. Pia nakala ilitumwa NEC na kupokelewa kwa diapatch siku hiyohiyo 1/12/2020 saa saa 7:12 mchana.

Kwa kuwa Tulia ametamla kwamba ikiwa akina Kishoa wamefukuzwa uanachama hawapaswi kuwepo bungeni, basi apitie mafaili hapo ofisini ataona barua ya Chadema iliyotumwa 1/12/2020 halafu afanye maamuzi kwa mujibu wa Katiba.
Baada ya hapo jopo la wanasheria wa Chadema liwaburuze mahakamani Bwana Ndugai na Bibi Tulia kwa kutumia rasilimali za umma kulipa mishahara, posho na marupurupu kwa watu wasio wabunge kwa miezi 6. Huu ni uhujumu uchumi.!





Comment


Share
 

Hata ww boss wako anaweza tu kusema nakupa kazi na kila salary yako lazima unipe laki tano na akaandika kwenye mkataba kufanya ni halali while ni haramu
 
Kituko! Mhemiwa kishoa ni sawa na mtuhumiwa anaekiri kosa mahakamani kuwa nimeiba, na Mheshimiwa naibu spika naye ni sawa na hakimu anaemwambia mkosaji mwizi, usiseme nimeipa!

Hakuna shida yoyote, tuache wivu wa maendeleo, wale wamepata acha wale
 
Mimi naona bunge lote lingevunjwa tu! Ili mishahara na posho zao, serikali itumie kuwakopesha wajasiriamali, wakulima na wafanyakazi kwa riba ndogo!

Maana hata hao wabunge walio wengi wa ccm na wale wawili wa upinzani, wameingia humo bungeni kwa magumashi tu.
 
Maskini!!!!!!!!, Betina anatafuta aibu tupu.
Tumeuona MKONO wa Mungu tulipokuwa tunapita katika bonde la uvuli wa mauti.
Nyakati za ubabe mbuzi zimekwisha na kwenda nae mkuu wa takataka hizo.
Bunge sio mali binafsi ya Spika wala aliyekalia au kukalishwa kwenye kiti hicho.
AMEN
 
Spika mwemyewe naye mwizi wa kura vilevile patam hapo - mwizi na mwizi wanapokutana uso kwa uso.
Samahani, nilikua nikimaanisha mtuhumiwa mwizi na hakimu mwizi
 
Kosa lake nn? Unadhan kakurupuka? Au anaelewa in and out kuhusu kutokua na chama. Hivi mikutano ya kisiasa ikianza watasimama majukwaani kama wabunge wa chama gani? Na je watavaa sare za chama gani? 🤣🤣🤣🤣👇👇! Think about it
Mbunge hajielewi kabisa
 
Kishoa ushaambiwa huwa chama humo sepa !! Nchi hii ina vituko aisee..huwezi amini. Huyo mwingine na yeye aliyetolewa gelezani usiku wa manane kuwahi saa mbili asubuhi kuuapia Ubunge - katulia as if nothing illegal happened.
Ndugai ameharibu sn hii nchi
 
That was a Freudian slip.

La uvundo halina ubani.
 
Ungefahamu kuwa hauna HOJA ungejipumzikia tu. Bahati mbaya buku 7 zinakuswaga.
 
Wakati Katiba inaongelea uhuru wa kukutana, sio vikao tu, bali hata mikutano ya hadhara, sheria ya vyama vya siasa inafafanua kwamba vyama vina haki ya kufanya mikutano ya hadhara, maandamano, na kuipinga serikali iliyoko madarakani.

Sasa Naibu Spika anapopotosha makusudi, ana maanisha kusema nini haswa? Ni AIBU kubwabkwa mwanasheria wa kiwango chake kupotosha taifa na kulidanganya bunge mchana kweupe.

Na kwa hili suala la wabunge 19 wa "Changamoto ya upumuaji" a.k.a. covid-19, Inajulikana wazi kwamba hao wapo bungeni kwa mgongo wa Magu, aliyemwamrisha Spika. Ndugai peke yake asingemudu kuipika hiyo pilau. Swali ni je, Tulia anataka kusema ule mgongo wa Magu ume eksipaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…