Naibu Spika Dkt. Tulia: Jesca Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya Spika haina taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako

Naibu Spika Dkt. Tulia: Jesca Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya Spika haina taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako

Nafkiri amejuta kusema walifutwa uanachama gafla hiyo kauli mara ingemlaza na njaa lakini Naibu spika amempenda kumpa tena nafasi kufuta kauli, kumbe hawa Covid19 wanajua fika wapo bungeni kwa msaada wa Spika tu sio vyenginevyo, siku Ndugai akiamka vibaya wataenda zao nje
Wewe nimekuelewa, hao jamaa wanalindana kiaina.
 
Kutafanyika kikao kati ya Ndugai, Mbowe na Mahera chini ya mshauri wa Rais wa mambo ya siasa kujua " Kwanini Halima James Mdee wako bungeni bila ridhaa ya kamati kuu ya Chadema ?"

Mjue wale wameapa mbele ya spika, na tume ya uchaguzi ndio ilipeleka majina kwa spika,

Na wale wako bungeni ni kwa because sababu zilizotumika kuwavua uanachama hazina mashiko

Ni sawa na ambavyo Mbowe Aliamua kuwatoa wabunge wote bungeni kisa ni corona wakati bunge linaendelea
 
Mbona Mbowe alikuwa anakula 1.5 za viti maalum miaka yote? So ni poa tu kwa ndugai
Hizo ni stori zenu wakati mnakuna nazi.
tapatalk_1576643810730.jpg
FB_IMG_1593760875709.jpg
 
Mjue wale wameapa mbele ya spika, na tume ya uchaguzi ndio ilipeleka majina kwa spika,

Na wale wako bungeni ni kwa because sababu zilizotumika kuwavua uanachama hazina mashiko

Ni sawa na ambavyo Mbowe Aliamua kuwatoa wabunge wote bungeni kisa ni corona wakati bunge linaendelea
Corona hiyo hiyo ikaondoka na mwenyekiti wenu
 
Corona hiyo hiyo ikaondoka na mwenyekiti wenu

Ww ndio ulikuwa Dr wake?
Tatizo mkishapata vitekno mnaanza kuandika vitu hata hamvijui

Leo ukiambiwa udhibitishe unaanza kulia na kusema unaonewa
 
Mbunge Kishoa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amelalamikia kunyimwa nafasi ya kufanya mikutano ya kisiasa kabla hajaondolewa kwenye chama chake. Naibu spika akalazimika kuingilia kwa kusema haihitaji kuwa naye bungeni kama hana chama cha Siasa kwani ni takwa la kuwemo bungeni.

"Mheshimiwa Naibu spika sitaki sana kubishana na kiti chako lakini niseme mimi ni miongoni mwa wahanga wakubwa sana wa suala hili la mikutano ya hadhara, nikiwa kama katibu mkuu wa Baraza la wanawake CHADEMA wakati huo kabla sijaondolewa kwenye chama changu...'' Alisema Kishoa

Spika alimkatisha na kusema, "Mheshimiwa Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya spika haina hiyo taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako, kama umeondolewa kwenye chama chako usingekuwa humu ndani kwa sababu wabunge waliokuwemo humu ndani wote wana vyama vya siasa ndivyo katiba yetu inavyosema na ndiyo katiba yetu inavyosema ile katiba hairuhusu mbunge ambae hana chama"

Kishoa: Mheshimiwa Spika hatujaondolewa kwenye chama, bado mimi ni mwanachama wa CHADEMA kwasababu tuko kwenye taratibu na tumekata rufaa na taratibu zinaendelea

Tulia: Mheshimiwa ngoja, waheshimiwa wabunge taarifa rasmi za Bunge ni kumbukumbu, umezungumza kabla ya sentesi yako ya sasakwamba kabla hujaondolewa kwenye chama chako, futa hiyo kauli kwanza halafu umalizie mchango wako kwasababu ndani ya bunge hili tutakuwa tunavunja katiba kama tutakuwa na wewe humu kama umeshaondolewa na chama chako

Kishoa: Mheshimiwa naibu spika nimefuta

Hoja ya Mbunge Jesca ilianzia kwenye haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na kukumbana na miongozo mingi kutoka kwa wabunge wakimtaka afute kauli. Kishoa amesema nchi ikiongozwa kwa matamko badala ya katiba itapotea.

Akifafanua kuhusu mikutano ya vyama vya kisiasa, Naibu spika amesema mikutano hiyo ipo kwenye katiba za vyama vya siasa na hufanyika kwa vipindi na sio ya hadhara akitolea mfano mkutano mkuu wa CCM uttakaofata utafanyika JK Convection centre na huo ndio unaitwa mkutano wa CCM lakini Rais akienda mahali unakuwa mkutano wa Rais na si CCM.

MY TAKE:

Je, CHADEMA haijatarifu bunge kuhusu kuwavua uanachama Wabunge 19 wa CHADEMA?

Zaidi soma: John Mnyika amuumbua Spika kwa kutoa ushahidi wa Ofisi ya Spika kupokea barua ya CHADEMA kuwavua ubunge wanachama wake
Kituko! Mhemiwa kishoa ni sawa na mtuhumiwa anaekiri kosa mahakamani kuwa nimeiba, na Mheshimiwa naibu spika naye ni sawa na hakimu anaemwambia mkosaji mwizi, usiseme nimeipa!
 
Mbona Mbowe alikuwa anakula 1.5 za viti maalum miaka yote? So ni poa tu kwa ndugai
Hata baada ya CAG kutogundua ubadhirifu wowote kuhusiana na fedha husika,Takukuru ilipewa jukumu la kuchunguza upya uhalali na matumizi ya fedha hizo ambazo zilikuwa zinachangwa kwa mujibu wa katiba ya Chadema,lakini Takukuru inaelekea waligonga mwamba,maanake wako kimya mpaka leo.
 
Katibu Mkuu wa chama CDM amelishalitaarifu Bungekuhusu hao covid 19, ni uhuni uhuni tu ndiyo unaofanyika kuichezea katiba na sheria za nchi.
 
Kituko! Mhemiwa kishoa ni sawa na mtuhumiwa anaekiri kosa mahakamani kuwa nimeiba, na Mheshimiwa naibu spika naye ni sawa na hakimu anaemwambia mkosaji mwizi, usiseme nimeipa!
Spika mwemyewe naye mwizi wa kura vilevile patam hapo - mwizi na mwizi wanapokutana uso kwa uso.
 
Back
Top Bottom