Naibu Spika Dkt. Tulia: Jesca Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya Spika haina taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako

kungekuwa na viti maalum vya wanaume leo Chadema hamna mtu angevuliwa ubunge. Mbowe, Lissu, Lema wangekuwa viti vya mbele kabisa bungeni sema ndio hivyo chama chetu hakiamini wanawake
 
Screenshot_20210423-144547_1.jpg
 
Nakuuliza tu mkristo mwenzangu Dr Tulia Ackson maana Jesca Kishoa amekiri kuwa waliondolewa Chadema lakini wewe ukamtaka afute ukiri wake.

Kimaandiko matakatifu wewe Dr Tulia umetenda dhambi kubwa kuliko Jesca Kafulila aliyeamua kuwa mkweli wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kazi Iendelee!
Hiyo tunaiita "Dr Tulia Ackson ameamua kumuwekea Jesca Kishoa maneno mdomoni" Nadhani hii dhambi italitesa sana bunge la Ndugai.
 
CHADEMA waje hapa,kumbe hawakupeleka taarifa kwa spika kuhusu kuwavua uanachama wale COVID 19?!Hili walitolee maelezo,sisi wananchi tunajua wale so wabunge.
 
kungekuwa na viti maalum vya wanaume leo Chadema hamna mtu angevuliwa ubunge. Mbowe, Lissu, Lema wangekuwa viti vya mbele kabisa bungeni sema ndio hivyo chama chetu hakiamini wanawake
Hata wewe ukitaka utapewa hivyo viti maalum kupitia kwa chakubanga
 
Mbunge Kishoa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amelalamikia kunyimwa nafasi ya kufanya mikutano ya kisiasa kabla hajaondolewa kwenye chama chake. Naibu spika akalazimika kuingilia kwa kusema haihitaji kuwa naye bungeni kama hana chama cha Siasa kwani ni takwa la kuwemo bungeni.

"Mheshimiwa Naibu spika sitaki sana kubishana na kiti chako lakini niseme mimi ni miongoni mwa wahanga wakubwa sana wa suala hili la mikutano ya hadhara, nikiwa kama katibu mkuu wa Baraza la wanawake CHADEMA wakati huo kabla sijaondolewa kwenye chama changu...'' Alisema Kishoa

Spika alimkatisha na kusema, "Mheshimiwa Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya spika haina hiyo taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako, kama umeondolewa kwenye chama chako usingekuwa humu ndani kwa sababu wabunge waliokuwemo humu ndani wote wana vyama vya siasa ndivyo katiba yetu inavyosema na ndiyo katiba yetu inavyosema ile katiba hairuhusu mbunge ambae hana chama"

Kishoa: Mheshimiwa Spika hatujaondolewa kwenye chama, bado mimi ni mwanachama wa CHADEMA kwasababu tuko kwenye taratibu na tumekata rufaa na taratibu zinaendelea

Tulia: Mheshimiwa ngoja, waheshimiwa wabunge taarifa rasmi za Bunge ni kumbukumbu, umezungumza kabla ya sentesi yako ya sasakwamba kabla hujaondolewa kwenye chama chako, futa hiyo kauli kwanza halafu umalizie mchango wako kwasababu ndani ya bunge hili tutakuwa tunavunja katiba kama tutakuwa na wewe humu kama umeshaondolewa na chama chako

Kishoa: Mheshimiwa naibu spika nimefuta

Hoja ya Mbunge Jesca ilianzia kwenye haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na kukumbana na miongozo mingi kutoka kwa wabunge wakimtaka afute kauli. Kishoa amesema nchi ikiongozwa kwa matamko badala ya katiba itapotea.

Akifafanua kuhusu mikutano ya vyama vya kisiasa, Naibu spika amesema mikutano hiyo ipo kwenye katiba za vyama vya siasa na hufanyika kwa vipindi na sio ya hadhara akitolea mfano mkutano mkuu wa CCM uttakaofata utafanyika JK Convection centre na huo ndio unaitwa mkutano wa CCM lakini Rais akienda mahali unakuwa mkutano wa Rais na si CCM.

MY TAKE:

Je, CHADEMA haijatarifu bunge kuhusu kuwavua uanachama Wabunge 19 wa CHADEMA?
Hii ni planned movie....speaker wamempanga Jesca aongee wapate pa kuanzia
 
Kama hawajatimuliwa, hiyo idea ya kusema hadharani bungeni kuwa alifukuzwa imekujaje akilini kwake?? Daima ukweli haufichiki milele.

Ukweli una tabia ya kujipendekeza kutoka nje hata kama hutaki utoke. Ipo siku tu utakuponyoka na watu wataujua ukweli huo bila hiari yako!
 
Rais Samia Suluhu, Mungu ambariki sana huyu mama! Kweli uchungu wa mwana aujua Mama Mzazi. Kwa hotuba ya Rais SSH jana Bungeni, she's gonna reverse the situation completely!!! Tayari imeonesha nia ya kukutana na vyama pinzani kujadili huu upuuxi wa Wabunge 19 wa Ndugai na Kigagula Tulia..............!!!!
Yajayo yanafurahisha.
A.K.A betina wa nzoovweee
 
Sidhani....Nahisi Kuna namna alitaka kuchokonoa mada na amefanikiwa kwa kiasi fulani.

Alichofanya Kishoa ni kuionyesha Dunia kuwa sisi kuwemo humu ndani sio kwa mapenzi yetu ila Kuna nguvu iliyonyuma yetu.
Ndugaye leo kaumbuka
 
Waswahili wanasema "Mficha maradhi, kifo humuumbua"
Vitabu vitakatifu vinasema "Dhambi huua na huumbua mtu hadharani" 'Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo huvunjika bila kupata dawa"
 
Back
Top Bottom