Naibu Spika Dkt. Tulia: Jesca Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya Spika haina taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako

Naibu Spika Dkt. Tulia: Jesca Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya Spika haina taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako

Tulia endelea kuwafanganya wananchi. Halima mdee kwà mfano 2025 anaelekea wapi? Na kwà chama gani?au utampa jumbo la mbeya mjini? Halima bado ni mdogo kwà umri na hana ajira nyingine ataelekea wapi? Bora uwaeleze mapema kuwa hawana chama ilinwaanze kuhipanga kisiasa na kimaisha. Wengine waanze kuolewa au la
maisha yake yote hajawahi kufanya kazi zaidi ya ubunge katoka tu chuo akala ubunge viti maalumu kwa hiyo kaona ni halali yake na dharau kwa mbowe aliyemfikisha hapo
 
Huyo mbunge hajielewi, kawaida adhabu inapotolewa kinachofuatia ni utekelezaji, rufaa hukatwa ambapo huwa mtu anaendelea kutumikia adhabu yake, sasa kama hawa wabunge walivuliwa uanachama inamaana wamepoteza sifa ya kuendelea kukaa bungeni, kama itatokea washinde rufaa yao ndio watarudi bungeni kupitia chama chao.

Spika anajua hili kwani alishalifanya kwa wengine, Naibu spika nae anajua hili, ila wameamua kupindisha sheria makusudi kwa manufaa yao binafsi, unless otherwise tuambiwe kama Chadema hawakuandika barua kuijulisha ofisi ya Spika juu ya uamuzi wao wa kuwavua uanachama hao wabunge, jambo ambalo nitakuwa mgumu kuliamini.
 
Je, kuna uwezekano kwamba kila mwezi Ndugai anachukua mgao wake toka kwa COVID-19?
Inawezekana kabisa maana ndugai ni mjuzi wa kutengeneza fursa ya kufisidi.

Refer ile bili ya tiba yake India iliyompa sifa ya kuwa mgonjwa ghali zaidi duniani!!!
 
Kwani VAR inasemaje?
images (11).jpeg
 
Nakuuliza tu mkristo mwenzangu Dr Tulia Ackson maana Jesca Kishoa amekiri kuwa waliondolewa Chadema lakini wewe ukamtaka afute ukiri wake.

Kimaandiko matakatifu wewe Dr Tulia umetenda dhambi kubwa kuliko Jesca Kafulila aliyeamua kuwa mkweli wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kazi Iendelee!
 
Naibu Spika ni Mwanasheria wa Kiwango cha PhD,
anajua kabisa kuwa Tanzania haina Mgombea Binafsi tangu 1958 ambao Chief Sarwat alishinda Ubunge wa Mbulu kama Mgombe Binfasi baada ya kutofautiana na TANU na kwa mujibu wa Katiba yetu huwezi kuwa Mbunge kama huna udhamini/ hujapendekezwa na Chama cha Siasa; kama ilivyofafanuliwa na ibara ya 67(1) na (2)(e) na kwa kutambua hilo, ndio maana amehakikisha hansard isihifadhi mchango wa mtu ambaye anasema kuwa ameondolewa kwenye Chama chake na bado yupo Bungeni isipokuwa amesahau kuwa vicitm anasema amekata rufaa. Mtu akihukumiwa kifungo cha miezi5 huanza kuitumikia adhabu hapo hapo hata kama amekata rufaa na anao uwezekano wa kushinda. Kwenye malengo 17 Endelevu ya Dunia, lengo Na 16 ni kujenga TAASISI imara badala ya watu imara, Je Vyama vyetu vya Upinzani ni taasisi imara au ni watu IMARA kama Mbowe au Lipumba?

Ni wajibu wa NCHI kujenga Taasisi imara kama waasisi wa Nchi hii walivyojenga MAJESHI yetu yaliyo imara ambapo wanajeshi hupata Vyeo vyao kwa MERITS na sio kubebwa au kupendelewa. Vivyo hivyo, NGOs zetu nazo ziwe ni Taasisi imara kama Makanisa ya KKKT or RC.

Hongera Dr Tulia kwa kuweka record sahihi kuwa Ofisi ya SPIKA haina taarifa rasmi za kufukuzwa UANACHAMA wa Mhe Jesca, katika muktadha wa kisheria ni wajibu wa CDM kumprove
wrong Naibu spika kwa kuonyesha Dispatch book kuwa barua yao ilipokelewa tarehe ngapi, na nani,saa ngapi na mahali gani/Dodoma au Dar?

Nchi yetu imeheshimika Duniani kwa kuitii na kuilinda KATIBA yetu, tusiruhusu wanasiasa wakaanza kuinyofoa nyofoa kwa maslaji yao ya Muda mfupi; Katiba ni roho(soul) ya Taifa, huanzisha Ofisi na kuziwekea mipaka ili kudhibiti tabia na hulka zetu wanadam.
Kazi iendelee kwa Jina la JMT
 
Mbunge Kishoa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amelalamikia kunyimwa nafasi ya kufanya mikutano ya kisiasa kabla hajaondolewa kwenye chama chake. Naibu spika akalazimika kuingilia kwa kusema haihitaji kuwa naye bungeni kama hana chama cha Siasa kwani ni takwa la kuwemo bungeni.

"Mheshimiwa Naibu spika sitaki sana kubishana na kiti chako lakini niseme mimi ni miongoni mwa wahanga wakubwa sana wa suala hili la mikutano ya hadhara, nikiwa kama katibu mkuu wa Baraza la wanawake CHADEMA wakati huo kabla sijaondolewa kwenye chama changu...'' Alisema Kishoa

Spika alimkatisha na kusema, "Mheshimiwa Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya spika haina hiyo taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako, kama umeondolewa kwenye chama chako usingekuwa humu ndani kwa sababu wabunge waliokuwemo humu ndani wote wana vyama vya siasa ndivyo katiba yetu inavyosema na ndiyo katiba yetu inavyosema ile katiba hairuhusu mbunge ambae hana chama"

Kishoa: Mheshimiwa Spika hatujaondolewa kwenye chama, bado mimi ni mwanachama wa CHADEMA kwasababu tuko kwenye taratibu na tumekata rufaa na taratibu zinaendelea

Tulia: Mheshimiwa ngoja, waheshimiwa wabunge taarifa rasmi za Bunge ni kumbukumbu, umezungumza kabla ya sentesi yako ya sasakwamba kabla hujaondolewa kwenye chama chako, futa hiyo kauli kwanza halafu umalizie mchango wako kwasababu ndani ya bunge hili tutakuwa tunavunja katiba kama tutakuwa na wewe humu kama umeshaondolewa na chama chako

Kishoa: Mheshimiwa naibu spika nimefuta

Hoja ya Mbunge Jesca ilianzia kwenye haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na kukumbana na miongozo mingi kutoka kwa wabunge wakimtaka afute kauli. Kishoa amesema nchi ikiongozwa kwa matamko badala ya katiba itapotea.

Akifafanua kuhusu mikutano ya vyama vya kisiasa, Naibu spika amesema mikutano hiyo ipo kwenye katiba za vyama vya siasa na hufanyika kwa vipindi na sio ya hadhara akitolea mfano mkutano mkuu wa CCM uttakaofata utafanyika JK Convection centre na huo ndio unaitwa mkutano wa CCM lakini Rais akienda mahali unakuwa mkutano wa Rais na si CCM.

MY TAKE:

Je, CHADEMA haijatarifu bunge kuhusu kuwavua uwanachama Wabunge 19 wa CHADEMA?
Wewe ni mpumbaf kama wapumbaf wengine hasa hao kina covid -19.

Nani kakwambia kuwa hao ni wabunge wa cdm?mbona mnalazimisha kiki za kubumba bumba namna hiyo?
 
Kishoa ushaambiwa huwa chama humo sepa !! Nchi hii ina vituko aisee..huwezi amini. Huyo mwingine na yeye aliyetolewa gelezani usiku wa manane kuwahi saa mbili asubuhi kuuapia Ubunge - katulia as if nothing illegal happened.
Lawama zoote sasa atazibeeba Ndugaye naada ya boss wake kutangulia mbele ya haki.
 
Back
Top Bottom