Naibu Spika: Kuna watumishi wa TASAF bado wanaingiza ndugu zao kwenye Malipo

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
DODOMA: Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amesema kuna Watu wasio na sifa lakini wameingizwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kinyume na malengo ya mpango huo.

Akijibu taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwan Kikwete kuhusu uendeshaji wa TASAF, Zungu amesema "Kuna watu bado wanaingizwa kwa upendeleo, kuna mama wa miaka 70 kwenye Kata yangu Ilala wamekata Rufaa wamekataliwa, na hii inaelekea ni nchi nzima"

Aidha, Naibu Spika ameitaka Serikali kuhakikisha wanaoingizwa katika mpango huo ni wenye sifa na sio watumishi wa TASAF kuwaingiza ndugu zao ili wanufaike na Fedha za Wazee

Fuatilia Bunge Live hapa LIVE - Joseph Musukuma: Kikokotoo kinawaumiza wananchi, tunatengeneza taifa la wezi
 
Kuwa na umri wa miaka 70 hakiwezi kuwa kigezo Cha umasikini!
Kaya za wanufaika wa TASAF zilipatikana kwenye mikutano ya vijiji na Miata kwa wananchi kuwapitisha wenye sifa stahili!
 
Back
Top Bottom