Naibu Spika Tulia Ackson athibitisha Mbunge mmoja kupata maambukizi ya COVID-19

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema kuwa mmoja wa Wabunge wa Bunge hilo amethibitika kuwa ana maambukizi ya Virusi vya Corona.

Amesema mbunge huyo anaendelea vizuri na Serikali inaendelea kumuangalia na kumpatia matibabu stahiki. Kwa mujibu wa maelezo ya mbunge huyo ni kwamba alisafiri kwenda Dar es Salaam siku za karibuni, na aliporejea Bungeni siku ya Jumatano alianza kujisikia dalili kama zilizotangazwa na wataalamu kuhusu Virusi vya Corona na baadaye alithibitishwa kupata maambukizi ya Corona.

 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Tunusuru Na Corona Virus Diseases 19 Inatumaliza
 
Haina haja kuogopa. Corona ni kagonjwa kadogo sana. Haina haja kupaniki, tuendelee kuchapa kazi tu. Uchumi wetu ni mzuri na by the way kuna nchi 8 zinategemea nchi yetu kwa bidhaa zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…