Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge imependekeza kufanyika maboresho ya muda wa kutambulisha wageni waalikwa bungeni ambapo imetaja watakaotambulishwa ni wageni wa kitaifa, kimataifa pamoja na wageni waliotoa mchango kwa Taifa pekee.
Hayo yamesemwa leo Juni 11, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.
Zungu amesema utambulisho wa wageni wote bungeni huchukua muda mrefu, hali inayosababisha kuathiri muda uliotolewa kwa shughuli muhimu za Bunge.
Zungu amesema utambulisho wa wageni wote bungeni huchukua muda mrefu, hali inayosababisha kuathiri muda uliotolewa kwa shughuli muhimu za Bunge.