Naibu Spika, Zungu: Baadhi ya wageni wasitambulishwe bungeni

Naibu Spika, Zungu: Baadhi ya wageni wasitambulishwe bungeni

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge imependekeza kufanyika maboresho ya muda wa kutambulisha wageni waalikwa bungeni ambapo imetaja watakaotambulishwa ni wageni wa kitaifa, kimataifa pamoja na wageni waliotoa mchango kwa Taifa pekee.

Hayo yamesemwa leo Juni 11, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.

Zungu amesema utambulisho wa wageni wote bungeni huchukua muda mrefu, hali inayosababisha kuathiri muda uliotolewa kwa shughuli muhimu za Bunge.

Oia na kumsifia Mama iondolewe ina kula muda mwingi sana
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge imependekeza kufanyika maboresho ya muda wa kutambulisha wageni waalikwa bungeni ambapo imetaja watakaotambulishwa ni wageni wa kitaifa, kimataifa pamoja na wageni waliotoa mchango kwa Taifa pekee.

Hayo yamesemwa leo Juni 11, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.

Zungu amesema utambulisho wa wageni wote bungeni huchukua muda mrefu, hali inayosababisha kuathiri muda uliotolewa kwa shughuli muhimu za Bunge.

😁😁😁 hivi huyo zungu ni mtanzania? 😁😁😁 nchi inajitia utumwani yenyewe kwa kujitakia....tatizo ni kukosekana kwa daraja za uraia ...huyo zungu alitakiwa kuwa na uraia wa daraja ya tatu ...ambao usinge ruhusu hata kupiga kura au kuwa mwanasiasa a7 mfadhiri wa kisiasa...na wenzake kina ponjori na kina rostam
 
Wanafanya vitu, mpaka wanaona aibu wenyewe. Bunge walilifanya kama guest house za uchochoroni. Eti mgeni wa mbunge, ukute ni hawara yake. Wewe mwenyewe usionekane bunge lijalo. Ni kati ya wabunge mizigo tu.
Kabisa manake ilifika wakati uholela ulizidi unakuta eti Wageni wanatambulishwa ni Wageni wa mbunge flani wakati huyo mbunge mwenyeji mwenyewe pale bungeni hayupo.
Kuna watu walikuwa wanatoa.conection mtu apewe mwaliko wa.kufika bungeni ,yaani jina la.mbunge linatumika kumwalika.mtu bungeni wakati huyo mbunge hata hamfahamu huyo mgeni wake
Naona wameshtuka ujinga wao mtu anatambulishwa ni mgeni wa mbunge flani wakati huyo mbunge hayupo hapo kwenye kikao
 
hili jengo limejengwa kwa nssf zetu na hazijawahi kulipwa tuna haki ya kuingia na watupe na chai kabisa, wabunge wamechaguliwa na wananchi hivyo kila mwananchi ni mgeni wa kitaifa. ila sio mbaya mwakani harudi atakuwa anawaona kwenye luninga
 
Madhara ya uchawa ndiyo yamefikisha hapo bunge.
Maana kila mtu kutaka sifa kutambulishwa bungeni.

#UPDATES Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge kupitia Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu, imependekeza kufanyika maboresho ya muda wa kutambulisha wageni waalikwa bungeni ambapo imetaja watakaotambulishwa ni wageni wa kitaifa, kimataifa pamoja na wageni waliotoa mchango kwa Taifa pekee.

Wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo Zungu amesema utambulisho wa wageni wote bungeni huchukua muda mrefu, hali inayosababisha kuathiri muda uliotolewa kwa shughuli muhimu za Bunge. #EastAfricaTV
IMG_1580.jpeg
 
Kutambulisha wale wageni ilikuwa vituko sana! Mara wanafunzi wa shule msingi, mara wapiga kura wa mbunge, mara wasanii wa bongo muvi. Kutambulisha ilipoteza muda sana
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge imependekeza kufanyika maboresho ya muda wa kutambulisha wageni waalikwa bungeni ambapo imetaja watakaotambulishwa ni wageni wa kitaifa, kimataifa pamoja na wageni waliotoa mchango kwa Taifa pekee.

Hayo yamesemwa leo Juni 11, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.

Zungu amesema utambulisho wa wageni wote bungeni huchukua muda mrefu, hali inayosababisha kuathiri muda uliotolewa kwa shughuli muhimu za Bunge.

Bora, maana mtu anabeba machawa wake, mara wake zake wanne na wasanii wake anaenda kuwatambulisha bungeni, hovyo kabisaa
 
Bora watambulishe tu wageni hadi muda uishe, maana hamna cha maana huwa huo mkutano wa wachumia tumbo hujadili.
 
Back
Top Bottom