Naibu Spika Zungu: 'Vijana epukeni ngono kabla ya ndoa'

Naibu Spika Zungu: 'Vijana epukeni ngono kabla ya ndoa'

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amelitaka Bunge la Vijana kutoka na azimio ambalo litawaasa vijana kujiepusha na masuala ya ngono kabla ya ndoa.

Zungu ameyasema hayo leo Alhamisi Disemba Mosi, 2022 wakati akifungua Bunge la Vijana ambalo limeanza vikao vyake vya siku tano katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini hapa.

Amesema wakati dunia inaadhimisha siku ya ukimwi, maambukizi kwa watu wazima yamepungua kwa kiasi kikubwa huku kwa vijana yakiongezeka.

“Vijana wengi mnafanya ngono si salama na kwanini ufanye ngono huna mke wala mume biblia na quran inakataza uzinifu. Fuateni maadili,”amesema.

Aidha, amesema majukwaa kama bunge hilo yatawajenga vijana katika uongozi, ujasiri na uzalendo na kuwa wenye uwezo wa kujenga hoja.

Amesema lengo la Bunge hilo la vijana ni kuwawezesha kuwa na uelewa juu ya uendeshaji wa shughuli za bunge na kuwandaa kuwa viongozi wa baadaye.

Pia amesema lengo jingine ni kuwafundisha vijana utamaduni wa kuvumiliana, kubishana kwa hoja na kuheshimu mawazo ya watu wengine.

Naye Spika wa Bunge la Vijana Nchini, Antipas Pamba amewataka vijana wenzao kuhakikisha kuwa wanajikinga na maambukizi mapya ya VVU kwa kuepuka kufanya ngono kabla ya ndoa.

“Itakapotokea vijana wameingia majaribuni wakati hawajaoa wala kuolewa ingawa sishauri hivyo basi wafuate njia mbalimbali za kujikinga. Sisi katika vyuo vikuu Serikali inafanya jitihada ya kuleta vifaa kinga (kondomu) kwa ajili ya kuzuia maambukizi” amesema.

MWANANCHI
 
Hivi vitabu vya dini vinavyokagaza uzinzi ndio hivyo hivyo ambavyo vinasema kiwa siku za mwisho tutayaona haya tunayo yaona. Tuache unabii utimie. Watu wakulane tuu na ukimwi uwepo maana ilishaandikwa na hamna anayeweza zuia yaliyoandikwa kwenye vitabu vya dini.
 
na yeye haepuke kukurupuka kuongea ovyo bungeni ndio maana kasababisha tozo
 
Hivi vitabu vya dini vinavyokagaza uzinzi ndio hivyo hivyo ambavyo vinasema kiwa siku za mwisho tutayaona haya tunayo yaona. Tuache unabii utimie. Watu wakulane tuu na ukimwi uwepo maana ilishaandikwa na hamna anayeweza zuia yaliyoandikwa kwenye vitabu vya dini.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]lengo lako wachapane kavu kavu wafe?
 
Swali n kwamba yeye aliviepuka pia?
Mbna hazungumzii wao kuepuka kuitafuna nchi?
 
Back
Top Bottom