Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkutano huo wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji (International Transparency and Accountability Conference - ITAC) umefatika Septemba 28 na 29, 2023 ukiwa na lengo la kutoa elimu na kuibuka utatuzi wa changamoto za mazingira unatarajiwa kushirikisha Wadau 300 kutoka Nchi sita.
Akizungumza na Wadau mbalimbali walioshiriki kwenye mkutano huo hilo, Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande amesema:
“Tanzania kwa sasa ipo katika kiwango kizuri jinsi inavyoshirikiana na taasisi mbalimbali juu ya kupambana na mabadiliko ya Tabianchi.”
Ameongeza kuwa “Madhara ya Tabianchi tunayaona kama hakuna usimamizi mzuri wa fedha na kuwajibika katika kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi.”
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovic Utoah amesema utaratibu wa kushughulikia maafa sio mkubwa, ili tufanikiwe tunahitaji fedha na hizo fedha zinapotikana basi zitumike kama ilivyopangwa, kwa uwazi na uwajibikaji.”
Video: Azam TV