Super Sub Steve
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 17,404
- 10,900
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naibu waziri wa maji mh Awesu amesema atawalipia kiingilio mashabiki wote atakao wakuta uwanjani kesho katika mechi ya Stars na Uganda.
Awesu amesema atafika mapema uwanjani akiwa amevalia jezi za Stars na unachotakiwa kufanya ni kumkimbilia na kumshika mkono tu basi mtaingia naye ndani ya uwanja.
Vijana changamkieni fursa hiyo mkaishangilie Taifa Stars
Source Clouds 360 on saturday
Maendeleo hayana vyama!
Hahahaa....... Wabongo bhana!Sasa kiingilio chenyewe ni shilingi 2000! halafu mtu anataka kujichukulia ujiko kwa kodi zetu. Bila shaka hizi ni zile hela anazozipata kupitia posho za kuzurura mikoani kila siku kukagua miradi yao ya maji.
Mkuu basi na wewe walipie baadhi!
Waganda wa kawaida? Tafadhali rejea kauli yako hii jumapili saa 3 usiku
Wameleta kikosi mbadala!Waganda wa kawaida? Tafadhali rejea kauli yako hii jumapili saa 3 usiku
Kuishangilia Taifa Stars mwisho wake huwa disappointment
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani.Awamu hii tutashuhudia mengi ya kushangaza kama sio kustaajabisha. Watu tunasubiri kunywa beer za nusu bei baada ya 'ushindi'wa stars
Sent using Jamii Forums mobile app
Anajifanya Yesu kwamba ye ndo mkate na divaikushika Mkono anamsnisha unachukua pesa
Yaani sisi Tanzania, ili tuelekee Cameroon, inatakiwa tuwe na maombi matatu tu.Jamani hizo mbwembwe muwe mnakumbuka kufanya mambo na Lesotho ifungwe la sivyo watu watakunywa bia za nusu bei na kusonga mbele tusisonge!!
Serena hotel nusu bei ruksa!Yaani sisi Tanzania, ili tuelekee Cameroon, inatakiwa tuwe na maombi matatu tu.
1. Kumuombea Lesotho afungwe.
2. Kujiombea sisi wenyewe tushinde, huku tukiomba Ombi namba 1 lipokelewe na MUNGU BABA.
3. Kujiombea sisi tutoe sare, huku tukiomba Ombi namba 1, lipokelewe na MUNGU BABA.
*Lesotho wao watakuwa na maombi Mawili tu*
1. Kuiombea Tanzania ishinde na wao Lesotho Washinde
2. Kuiombea Tanzania itoe sare na Lesotho wao watoe sare.
Utagundua kuwa Maombi ya Lesotho hayana ubaguzi, na wanarejea ile maneno ya Biblia yanayosema *Mpende adui yako kama unavyojipenda Mwenyewe*
Wakati sisi tunatumia Maombi sijui ya Kitabu gani, ya kumuombea adui mabaya.
*N.B* ```Yaani hata itokee sisi tukashinda magoli 10 kwa sufuri hata magoli 100, halafu Lesotho akashinda kamoja tu (1) Basi sisi tutabaki kuwa wapenzi watazamaji wa michuano wakati Lesotho Washiriki wa michuano```
*Cape Verde yeye atakuwa na maombi mawili tu*
1. Kujiombea wenyewe Cape Verde washinde
2. Kuiombea Tanzania Ifungwe, huku wakiomba ombi namba 1, lipokelewe na MUNGU BABA.
3. Kuiombea Tanzania itoe sare, huku wakiomba ombi namba moja lipokelewe na MUNGU BABA.
*Msimamo wa kundi ni hivi*
*Timu.* *Alama*
1. Uganda............ 13
2. Lesotho........... 5
3. Tanzania......... 5
4. Cape Verde.........4
Mechi ziko hivi
Tanzania v Uganda
Cape Verde v Lesotho
```Hivi bajeti ya kufanya sherehe kama tukishinda imeshaandaliwa ama tutajua mbele ya Safari? Na Bar za kunywa vinywaji nusu Bei zimeshatajwa ama tutajua tukishinda?```
*Halafu naomba kuuliza tutafanya sherehe tukishinda tu ama tukifuzu?*
Mkuu nimecopy sehemu[emoji3]
Sent using Jamii Forums mobile app
Wabongo kwa kutengeza pesa za kupiga nadhani tunaongoza duniani. Uhamasishaji tumeshapiga pesa ya kufa mtu. Pesa siyo muhimu kitu muhimu kwasasa ni ushindi ndugu.Mzigo umetoka Vijana wanauchangamkia kuutafuna
Ukija kuskia gharama Za uhamasishaji Baada ya game utachoka
Hujui mpira wewe, Waganda wameshafuzu Afcon na mkononi wana mechi moja.