Naibu waziri Juma Awesu atoa ofa ya kuwalipia kiingilio mashabiki wote watakaowahi uwanjani kabla hajaingia Taifa Stars vs Uganda

Sasa kiingilio chenyewe ni shilingi 2000! halafu mtu anataka kujichukulia ujiko kwa kodi zetu. Bila shaka hizi ni zile hela anazozipata kupitia posho za kuzurura mikoani kila siku kukagua miradi yao ya maji.
 
Haya yote kisa 2000?.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kiingilio chenyewe ni shilingi 2000! halafu mtu anataka kujichukulia ujiko kwa kodi zetu. Bila shaka hizi ni zile hela anazozipata kupitia posho za kuzurura mikoani kila siku kukagua miradi yao ya maji.
Hahahaa....... Wabongo bhana!
 
Hivi wanaelewa kuwa Lesotho wakishinda mechi yao huko sisi hata tumfunge uganda 100 hatuendi mahali? Hizi motisha wangefanyaga kipindi kile
 
Kuanzia j3 tutaanza kusikia pongezi zikitumwa kwa mtukufu jiwe sihasa zitachukua nafasi na sifa sifa zitakua nyingi kwa hawa watu hawa bashite bora Uganda wafanye yao sisi tuendelee kua wapenzi watazamaji tu
Uzalendo wenye mipaka hauna tija kwa taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani hizo mbwembwe muwe mnakumbuka kufanya mambo na Lesotho ifungwe la sivyo watu watakunywa bia za nusu bei na kusonga mbele tusisonge!!
Yaani sisi Tanzania, ili tuelekee Cameroon, inatakiwa tuwe na maombi matatu tu.
1. Kumuombea Lesotho afungwe.
2. Kujiombea sisi wenyewe tushinde, huku tukiomba Ombi namba 1 lipokelewe na MUNGU BABA.
3. Kujiombea sisi tutoe sare, huku tukiomba Ombi namba 1, lipokelewe na MUNGU BABA.

*Lesotho wao watakuwa na maombi Mawili tu*

1. Kuiombea Tanzania ishinde na wao Lesotho Washinde
2. Kuiombea Tanzania itoe sare na Lesotho wao watoe sare.

Utagundua kuwa Maombi ya Lesotho hayana ubaguzi, na wanarejea ile maneno ya Biblia yanayosema *Mpende adui yako kama unavyojipenda Mwenyewe*
Wakati sisi tunatumia Maombi sijui ya Kitabu gani, ya kumuombea adui mabaya.

*N.B* ```Yaani hata itokee sisi tukashinda magoli 10 kwa sufuri hata magoli 100, halafu Lesotho akashinda kamoja tu (1) Basi sisi tutabaki kuwa wapenzi watazamaji wa michuano wakati Lesotho Washiriki wa michuano```

*Cape Verde yeye atakuwa na maombi mawili tu*

1. Kujiombea wenyewe Cape Verde washinde

2. Kuiombea Tanzania Ifungwe, huku wakiomba ombi namba 1, lipokelewe na MUNGU BABA.

3. Kuiombea Tanzania itoe sare, huku wakiomba ombi namba moja lipokelewe na MUNGU BABA.

*Msimamo wa kundi ni hivi*

*Timu.* *Alama*
1. Uganda............ 13
2. Lesotho........... 5
3. Tanzania......... 5
4. Cape Verde.........4

Mechi ziko hivi
Tanzania v Uganda
Cape Verde v Lesotho

```Hivi bajeti ya kufanya sherehe kama tukishinda imeshaandaliwa ama tutajua mbele ya Safari? Na Bar za kunywa vinywaji nusu Bei zimeshatajwa ama tutajua tukishinda?```
*Halafu naomba kuuliza tutafanya sherehe tukishinda tu ama tukifuzu?*
Mkuu nimecopy sehemu[emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serena hotel nusu bei ruksa!
 
Mzigo umetoka Vijana wanauchangamkia kuutafuna

Ukija kuskia gharama Za uhamasishaji Baada ya game utachoka
Wabongo kwa kutengeza pesa za kupiga nadhani tunaongoza duniani. Uhamasishaji tumeshapiga pesa ya kufa mtu. Pesa siyo muhimu kitu muhimu kwasasa ni ushindi ndugu.
 
Hizi hamasa zote hata SIJUI faida yake ni NINI? Tulipaswa tungeaza KUHAMASISHA toka tulipoanza kucheza ktk kundi letu! Mf Simba walivyojiwekea malengo ya kushinda mechi zote za ugenini! Na wakafanikiwa kufika robo fainali! Sasa kama timu yetu ya TAIFA ingeshinda mechi zote za nyumbani TUNGEKUWA na UHAKIKA bila ya kutegemea matokeo mengine! ( Kama NITAKUWA SAHIHI Ili tuvuke tumfunge mganda halafu Lesotho afungwe au adroo! Lkn tukimfunga mganda na Lesotho akishinda tumetoka) Sasa TUJUWEKEE utamaduni kila timu zetu zinapoingia ktk mashindano bc kuwe na UHAMASISHAJI MKUBWA ITATUSAIDIA SANA,! MUNGU IBARIKI TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…