Naibu Waziri Katimba: Rufiji Imepata Mafanikio Makubwa

Naibu Waziri Katimba: Rufiji Imepata Mafanikio Makubwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amepongeza jitihada za maendeleo zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta ya Elimu,Afya na miundombinu ya Barabara za Mijini na Vijijini.
GesxqEcXcAAu0NY.jpg

Mhe. Katimba ametoa pongezi hizo leo Tarehe 13 Disemba 2024 wakati akitoa salamu zake kwa wananchi wa Ikwiriri wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Bibi Titi Mohamed katika uwanja wa Ujamaa Ikwiriri wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani.
GesxqEbXIAA6gFx.jpg

Mhe. Katimba amesema mbunge wa jimbo la Rufiki ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wa jimbo hilo wanapata maendeleo na kuifanya Rufiji kuwa na mabadiliko ndani ya muda mfupi jambo ambalo limekuwa alama isiyosahaulika kwa wananchi wa jimbo hilo.
GesxqEUW0AAv2Wn.jpg

Katika hatua nyingine Mhe. Katimba amewapongeza wananchi wa Rufiji kwa ushiriki mzuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
GesxqEVWcAAfh-X.jpg
 
Back
Top Bottom