Naibu Waziri Kihenzile: Sekta Binafsi Kuingia Kwenye Usafirishaji wa Reli (MGR & SGR)

Naibu Waziri Kihenzile: Sekta Binafsi Kuingia Kwenye Usafirishaji wa Reli (MGR & SGR)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko leo Oktoba 01, 2024 amezindua usafirishaji wa bidhaa mbichi zikiwemo mbogamboga na matunda kwa treni, kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam.

Uzinduzi huo umefanyika katika stesheni ya Reli ya Zamani (MGR) ya Kilosa mkoani Morogoro, ambapo TRC imeanza kufanya usafirishaji huo kwa mabehewa nane iliyopewa msaada na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na baadae Serikali inalenga kuongeza mabehewa mengine 264 na hivi karibuni usafirishaji huo utahamia kwenye Reli ya Kisasa (SGR).

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema katika kuhakikisha huduma ya usafirishaji mbogamboga, nyama na matunda kwa njia ya treni ambayo imezinduliwa leo Kilosa mkoani Morogoro inakuwa endelevu, ya uhakika, yenye gharama nafuu na yenye kuzingatia mahitaji ya wateja, wanawakabirisha watu na sekta binafsi kushirikiana na Serikali kuendesha huduma hiyo.

"Serikali inatoa hamasa na kuwakaribisha watu binafsi ambao wana nia ya kuwekeza na kushirikiana na Serikali katika jambo hili kuchangamkia fursa kuwekeza katika eneo hili ambalo lina tija kubwa kiuchumi",

"Serikali imeshaweka mazingira wezeshi ya biashara kwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Reli ya mwaka 2017 ili kuruhusu watu binafsi kutumia miundombinu ya reli kutoa huduma za usafirishaji".

Kihenzile amesema hayo wakati akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko katika stesheni ya Reli ya Zamani (MGR) ya Kilosa mkoani Morogoro, wakati wa hafla ya kuzindua mkakati wa upatikanaji wa mizigo ili kuimarisha biashara ya usafirishaji nchini kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Screenshot 2024-10-01 at 17-35-53 @wizara_ya_uchukuzi • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-10-01 at 17-36-15 @wizara_ya_uchukuzi • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-10-01 at 17-36-41 @wizara_ya_uchukuzi • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-10-01 at 17-36-53 @wizara_ya_uchukuzi • Instagram photos and videos.png
GYyYkrNWYAEYQ1W.jpg
GYyYkrNWcAIMu7w.jpg
Screenshot 2024-10-01 at 17-33-22 Wizara ya Uchukuzi (@WizarayaUC) _ X.png
Screenshot 2024-10-01 at 17-32-43 Wizara ya Uchukuzi (@WizarayaUC) _ X.png
 
Good move
Ila Kwa nini wasingeenda Moja Kwa Moja kwenye treni ya umeme ,waweke cold storage ,zibebe maziwa ,nyama na mboga mboga toka dom na Moro
Halafu zikitoka Dar zibebe samaki fresh toka baharini kwenda Dom na Kilosa
 
Back
Top Bottom