Naibu Waziri: Madereva hatarishi wafutiwe leseni za udereva

Naibu Waziri: Madereva hatarishi wafutiwe leseni za udereva

Mapendekezo ya madereva wa kufutiwa leseni kwa Dar es salaam,njia za daladala,wanaotoka kigamboni kwenda Mkuranga na wale wanaotoka mwandege kigamboni, tukiweza kuanza na hao itakuwa salamu tosha kwa wale wa basi za mkoa[emoji848]
Na Kuna wa Chanika gongola mboto wanaendesha vibaya sana nao wamulikwe
 
Akizungumza na majeruhi wa ajali hiyo ambao 25 waliruhusiwa mara baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo na kuruhusiwa kuendelea na safari Sagini amewataka Wanachi kuhakikisha wanapaza sauti zao kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya mwendo kasi kwa madereva au wanapoona kusimama kwa safari mara kwa mara kutokana na ubovu wa magari wanayosafiria kwa kupiga namba za simu za Makamanda wa Polisi zilizopo ndani ya mabasi wanayosafiria
Changamoto zinaanzia hapa
  1. Kenye speed limit, hao madereva wanakula njama na askari wa usalama barabarani, wanatoa rushwa wanaruhusiwa kuwahi.
  2. Vibao vya 50 ni vingi mno na hata baadhi ya maeneo hakuna makazi ya wwatu, matokeo yake safari inawachosha abiria kiasi kwamba hawatoi ushirikiano mnaoutaka viongozi wa kupigia kelele mwendo kasi.
  3. Viongozi mngesafiri na public transport mngebaini changamoto nyingi za usafiri wa mabasi na ingekuwa rahisi kuzitafutia ufumbuzi, huu utaratibu wa kutumia taarifa za kusikia hautamaliza ajali na kuua abiria wengi.
  4. Ingeshauriwa mabasi yote na malori yote yafungwe dash cameras ili zisaidie kuwapa vyombo vya usalama picha halisi ya vyanzo vya alali na ndipo wanaweza kufungia leseni za madereva wazembe
 
Back
Top Bottom