Naibu Waziri: Madereva hatarishi wafutiwe leseni za udereva

Mapendekezo ya madereva wa kufutiwa leseni kwa Dar es salaam,njia za daladala,wanaotoka kigamboni kwenda Mkuranga na wale wanaotoka mwandege kigamboni, tukiweza kuanza na hao itakuwa salamu tosha kwa wale wa basi za mkoa[emoji848]
Na Kuna wa Chanika gongola mboto wanaendesha vibaya sana nao wamulikwe
 
Changamoto zinaanzia hapa
  1. Kenye speed limit, hao madereva wanakula njama na askari wa usalama barabarani, wanatoa rushwa wanaruhusiwa kuwahi.
  2. Vibao vya 50 ni vingi mno na hata baadhi ya maeneo hakuna makazi ya wwatu, matokeo yake safari inawachosha abiria kiasi kwamba hawatoi ushirikiano mnaoutaka viongozi wa kupigia kelele mwendo kasi.
  3. Viongozi mngesafiri na public transport mngebaini changamoto nyingi za usafiri wa mabasi na ingekuwa rahisi kuzitafutia ufumbuzi, huu utaratibu wa kutumia taarifa za kusikia hautamaliza ajali na kuua abiria wengi.
  4. Ingeshauriwa mabasi yote na malori yote yafungwe dash cameras ili zisaidie kuwapa vyombo vya usalama picha halisi ya vyanzo vya alali na ndipo wanaweza kufungia leseni za madereva wazembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…