Naibu Waziri Mahundi awatembelea majeruhi wa ajali Mbeya, apongeza huduma za Hospitali

Naibu Waziri Mahundi awatembelea majeruhi wa ajali Mbeya, apongeza huduma za Hospitali

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewatembelea majeruhi wa ajali iliyohusisha basi la CRN na Gari la miundombinu ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya iliyosababisha vifo vya watu wanne na majeruhi watano.

Snapinsta.app_472643690_18046870193362258_6884492945818382814_n_1080.jpg
Miongoni mwa majeruhi waliotembelewa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ni pamoja na Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya Lucia Sule, Waandishi wa Habari Epmacus Kalokola,Denis George na Seleman Ndelage.

Soma: Rais Samia ametoa zaidi ya TSh. Milioni 26 kwa Wahanga wa ajali Mbeya

Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amepongeza uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa namna wanavyopana kuokoa maisha ya majeruhi huku akipongeza Serikali ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan ilivyowekeza vifaa tiba hivyo kuokoa gharama kubwa kwenda hospitali nje ya Mkoa na nje ya nchi.

Snapinsta.app_482073906_18046870196362258_7779258925352878183_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom