Pre GE2025 Naibu waziri maji: Ukituma mbunge anayekubalika kwa mawaziri miradi ya maendeleo itajazana jimboni kwako

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Naibu waziri wa maji Andrea Methew amesema baada ya Njalu Silanga kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa wabunge wa CCM mkoa wa Simiyu ambapo utendaji wake ulipelekea Rais Samia kuridhia kutoa bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa maji kutoka ziwa Victoria huku akisema ndani ya jimbo hilo upatikanaji wa maji ulikuwa ni asilimia 58 mwaka 2021 na sasa upatikanaji wa maji ni asilimia 72.8.

Aidha amesema uwepo wa mbunge huyo ambaye anakubalika na kuheshimiwa wabunge wenzake pamoja na mawaziri ndiyo chachu ya kufanikiwa kwa miradi ya maendeleo jimboni humo.

Ameyasema hayo kwenye Mkutano Mkuu Maalum Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Itilima, mkoani Simiyu Februari 15, 2025 ambapo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akiwa ni mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu huo.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…