Naibu waziri mipango na uwekezaji: Makampuni ya mikopo wanaotoza riba kubwa kunyang'anywa leseni

Naibu waziri mipango na uwekezaji: Makampuni ya mikopo wanaotoza riba kubwa kunyang'anywa leseni

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Makampuni yanayojihusisha na mikopo umiza yameonywa kuacha tabia ya kutoa mikopo bila kufata utaratibu na kuishia kuumiza wananchi kwa kutoza riba kubwa.

Naibu waziri wa nchi ofisi ya raisi mipango na uwekezaji Stanslaus Nyongo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la ofisi za hazina ndogo zilizojengwa Katika kata ya bombambili manispaa ya Geita mkoani Geita.

Nyongo amezindua Jengo la hilo likiwa na thamani ya zaidi ya shillingi Bilioni 4.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa Jengo hilo lenye miundombinu ya kisasa leo Februari 17,2025 mshauri elekezi kutoka wakala wa majengo Tanzania ( TBA ) Mkoa wa Geita Amina Morsad amesema Jengo hilo limejengwa kwa thamani ya zaidi ya shillingi Bilioni 4 na limekamilika kwa asilimia 100 likiwa na Ofisi 14 na kumbi 2.

Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Constantine Kanyasu akiwa katika hafla hiyo licha ya kupongeza ujenzi wa Ofisi hizo ameiomba serikali kuboresha miundombinu ya Barabara kwa kiwango cha lami kwenda katika Ofisi hizo na Ofisi zingine za serikali zilizopo katika eneo hilo.

Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita katika uzinduzi wa Jengo hilo amesema serikali ya awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa kwa kujenga majengo ya kisasa Mkoani Geita.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mipango na uwekezaji Mhe Stanslaus Nyongo baada ya kuzindua Jengo la Ofisi hizo amesema serikali imeendelea Kuimarisha na kuboresha huduma za wizara ya Fedha ikiwemo kusogeza huduma hizo karibu na wananchi.
 
Vyumba 14 na kumbi 2 ni 4B!!!
Hebu tuone picha kwanza🙄
 
Back
Top Bottom