Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko ni Turufu Kuu ya Rais Samia katika kupata Kura nyingi za Kanda ya Ziwa

Hii nchi ikiongozwa na Majaliwa tutatoboa mapema mno.
Nikiambiwa nichague kati ya Majaliwa na Samia sitopoteza muda Kumchagua Samia kwakuwa Majaliwa kama Majaliwa ana Mapungufu mengi Kubwa likiwemo la Uwongo na lingine la ziada la Unafiki. Simkubali 100%
 
Nikiambiwa nichague kati ya Majaliwa na Samia sitopoteza muda Kumchagua Samia kwakuwa Majaliwa kama Majaliwa ana Mapungufu mengi Kubwa likiwemo la Uwongo na lingine la ziada la Unafiki. Simkubali 100%
Itifaki tu ndio ilimfanya ashindwe kusema kweli kwamba "Magu hatunaye duniani" ila tukija kwenye ufanisi Majaliwa yupo strict mno hata Mpango hamfikii.Majaliwa ni mwamba!
 
Ondoa hapo neno may be na jua ya kwamba Dotto Biteko ndiyo next Premier wa Tanzania kuanzia mwaka 2025.
Mi nakataa, kwa Yale MAELEZO yako pale naona kabisa huyu atatumika kupata kura 2025, baada ya hapo ni kupingwa teke kabisaa alafu watoto wakishua, walai wenzie waje washike nyadhifa muhimu wavune vya kustaafia... Ila sisi wa Kanda ya ziwa.. Hatutishwi na uteuzi huo.. Maana hauponyi maumivu ya Mpendwa wetu... 😁 😁
 
Umemsahau na yule wa nishati, bado huko wizarani mmetemwa mbaya, hii ni danganya toto ya kuletewa msumbwa
 
Hatutaki majizi ya kijani tena
 
Biteko anajibrand vizuri sana kwa 2025 kuwa PM.
 
Kanda ya ziwa sio ngumu kwa ssiem maana wakazi wa kanda hiyo 65%-70% ni wasukuma ambao ni bendera fata upepo ya ssem ,hata kama wangenyimwa huduma zote na watawala wakajakuambiwa "tunawapenda na tunawajali ndugu zetu " basi kazi kwisha sasa wahaya na wakurya na jamaa zao ni kinyume haki bin haki
 
Acha uongo wewe... Mimi nimezaliwa Usukumani na nimefanya kazi Usukumani tena nimeingia mpaka kule Bush ndani ndani... Wasukuma hawana Ukabila kabisa, mimi nimepokelewa Usukumani hakuna anayenijua ila nimepewa Misosi ya kila aina tena bure kabisa... Kidogo nipewe na mke ila nikakataa kwa sababu nilikuwa ninae mtoto mzuri.

Dotto Biteko mwenyewe ni msukuma, kazaliwa huko Geita. Na ni mbunge wa huko Geita. Kuhusu Angelina Mabula hakuna mtu anayeumia kwa sababu Angelina Mabula ni mbunge wa Mwanza mjini jimbo la Ilemela. Jimbo la Ilemela lina watu wa makabila mengi sana, kutolewa kwa Angelina Mabula hakuwezi kufanya watu wa Ilemela kukasirika.

Hapo kwenye Wasukuma na Ukabila umezingua, japo mimi sio msukuma. Wenye ukabila ni hayo makabila ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro huko ndiko kuna Ukabila, hao jamaa na wakenya tabia zao ni moja
 
Kongole Kwa kutumia Jicho la Tai kuona mwenendo wa Uchaguzi 2025..

MH NWM Biteko ni pia hana makundi yoyote kwahiyo MH Samia katumia hiyo karata kupata Kura za kutosha hasa Kanda ya Ziwa ambapo ndio sehemu pekee inayoamua Nani awe Rais kwa wingi wa Kura zao
 
Uko sawa kabisa...Je Dotto hawezi tumika kama Toilet paper?
 
Huu upuuzi wa kusema wasukuma wanasikitishwa na kuondokewa na mtu wao ukome kwani yeye alikua nani mpaka asife? Aliambiwa achukuwe tahadhari ya korona akaleta ujuaji akafa naona kama mnataka kuibeba kama agenda narudia tena huo ni upuuzi.
 
Inawezekana kweli amewekwa lwa lengo hilo lakini nachojiuliza mbona DB(Dotto Biteko) ni kama hana ushawishi katika kanda hii ya ziwa.

Kuhusu matola kutoamini kama kanda ya ziwa inaushawishi katika kura amekurupuka sana. Maana ni ukweli ulio wazi kuwa hii kanda ndiyo ina watu wengi sana na wenye misimamo yao, naomba usiwa underrate wasukuma mkuu matola hawa watu wana misimamo yao wakiamua huwafanyi kitu umedai wako mikoa mitatu tu kwa kutumia neno mwashita mimi nimekuelewa kuwa umemaanisha wapo mwanza, shinyanga na tabora kitu ambacho si sahihi

Japo wasukuma hawana ukabila kama ambavyo wewe unaona wanao lakini ndiyo kabila linaloenea kwa kasi ya ajabu katika nchi.

Mikoa ambayo naweza nikakutajia ina asilimia kubwa ya wasukuma ni Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Katavi, Mbeya, Kigoma, Morogoro, Rukwa, Kagera, Mara na hata Tanga karibia wilaya yote ya Kilindi ni wasukuma kwahiyo hao watu sio wa kubeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…