Rais Magufuli wakati yupo hai aliwaimarisha sana Wasukuma na kuwafanya wawe wamoja, sasa baada ya kufa walisambaa sana kama kondoo waliokosa mchungaji.
Sasa kule Kanda ya Ziwa Wasukuma bado wanaamini Magufuri hana mbadala, hawana habari kabisa na Rais Samia. Picha Hayati Magufuri bado zinatamba kwenye hoteli na saloon, wananchi wa kawaida bado hawapo na Rais Samia!
Sasa Rais Samia ametafakari vizuri kuwapelekea Biteko ili awakusanye awarejeshe kwenye ule umoja na kuwafanya waanze kuwa na imani nae na hii ndio kazi kuu ya Biteko, kuifanya Kanda ya Ziwa iwe mikononi na kuua kabisa Sukuma gang, maana kazi anayoifanya Waziri Mkuu Majaliwa ilikuwa haihtaji msaidizi.
Baba wa taifa hayati mwenye heri El Commandante JKN alikufa akituasa dhidi ya maadui 3:-
UJINGA
Nitamzungumzia adui huyu tu....
Raia ana dhima ya KULIPENDA TAIFA LAKE pamoja na TUNU ZAKE...
Ni wajibu wetu raia kujibidiisha KUSOMA....KUSIKILIZA WASOMI...KUTAFUTA HABARI ZA KISOMI....
Kisomo gani ?!!!
Kisomo cha kuitambua thamani kuu ya URAIA wake yakiwemo :-
✓Kuitambua serikali halali ,kwa kuipenda na kuitii.
Mh.Samia Suluhu Hassan ndiye RAIS wetu wa serikali halali ya JMT ,haihitaji hao baadhi ya wakazi wa kanda ya Ziwa kukumbushwa hayo.
✓Kuwaheshimu wateule wa Rais hata kama hawatoki miji yao.
It is high time now kwa vijana wenzangu akina komredi Patrobass Paschal Katambi na wengineo KUBUNI njia nyepesi za KUWASHAJIISHA ELIMU YA URAIA watu wao.
HITIMISHO:
Mh.Dotto Biteko ni Naibu Waziri Mkuu wa JMT akiteuliwa kwa sifa stahiki na kwa malengo ya kutuhudumia watanzania wenzake.
Mathalani leo hii ametukumbusha kuwa mikoa miwili (Dar na Pwani) inatumia jumla ya megawati 732 ,Dar es salaam ikitumia megawati 500 za gridi ya taifa kwa hiyo tuwe na hadi novemba/Desemba na uzalishaji wa bwawa la Mwalimu Nyerere wa megawati 2215 kupoozwa pale Chalinze kabla ya kuutumia hadi huko KANDA YA ZIWA [emoji120]
#Siempre JMT [emoji120]
#Mama Anaupiga Mwingi [emoji2956][emoji7][emoji2956]