DOKEZO Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwa Tanzania ataukosa huo Unaibu Wazili tu , ila kwa nchi zingine Angekamatwa nakufunguliwa mashtaka ya unyanyasaji na ukatili wakijinsia tena na hivi ni mwana CCM, intakaushiwa hadi itaisha hili lilikua ndo jambo la waandishi wa habali kukomali mpaka haki ya huyo kijana ipatikane, ila najua waandishi wa habali watapewa pesa mpaka itaisha kimyakimya. Na hilijambo limelichafua Taifa haswa kwa kufanywa na naibu wazili wa katiba na shelia je wengine hawafanyi zaidi ya hayo?
 
View attachment 2823504
Hashimu Ally Phillemon, mkazi wa Babati Mjini anaeleza kwamba alikamatwa eneo lake la kazi, Paleii Lake View Garden, mali ya mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba na kupigwa, kujeruhiwa na kuwekewa chupa katika maeneo ya haja kubwa.

Hashimu Ally anadai, Pauline Gekul alitoa bastola, akamueleza achague kukalia chupa mwenyewe au apigwe risasi na mwili wake wakautupe katika Ziwa Babati. Alipogoma, wakampiga sana, wakamuingizia chupa sehemu ya haja kubwa.

Hashimu Ally anasema alituhumiwa na bosi wake (Pauline Gekul) kutumwa kuweka sumu ili kumuua Pauline Gekul, tuhuma ambazo hazijathibitishwa popote hata na jeshi la polisi, akasulubiwa sana kisha kukabidhiwa polisi Babati na kumpiga kila siku asubuhi na jioni, kwa siku nne.

Hashimu Ally anasema alikana tuhuma zote hizo akiwa kituo cha polisi Babati Mjini na hata chini ya mikono ya mateso ya Pauline Gekul. Baada ya kupigwa kwa siku nne mfululizo akiwa polisi Babati, alidhaminiwa na baba yake mzazi lakini baadaye akaitwa ofisi za Manyara ili kutoa maelezo.

View: https://m.youtube.com/watch?feature=shared&v=04BSzpoa6xo

Hata hivyo, Mbunge Pauline kupitia Katibu wake alikanusha taarifa hiyo katika ujumbe uliowekwa kwenye mitandao ya kijamii ukimtuhumu Hashimu kufanya udanganyifu na kushirikiana na washindani wa Pauline wa kibiashara kumfanyia ushirikina na baadaye ujumbe huo kufutwa kwa maelezo kuwa suala hilo liko mikononi mwa Polisi.

Kusoma zaidi kuhusu majibu ya pauline ingia >> Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Saa chache baada ya tuhuma hizi kusambaa na kupigiwa kelele na wadau mbalimbali ikiwemo wa JamiiForums, Rais Samia Suluhu, jioni ya tarehe 25 Novemba 2023, ametengua uteuzi wa Naibu Waziri huyo wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Zaidi soma >> Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Watendaji wote wa CCM without exception ni changamoto
 
Nimesikitishwa na unyama uliotendewa huyo kijana. Ninashauri wafuatao nao wawajibike. (1) RPC wa Manyara (2) OCD wa Wilaya ya Babati (3) OCS wa Kituo cha Polisi cha Babati na Maaskari wote waliohusika kumtesa huyo kijana. Inakuwaje kijana anakaa Polisi muda wa siku nne akiteswa siku nne mfululizo bila dhamana. Hao wanatakiwa wafukuzwe kazi mara moja.
 
Maokoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukatili wa kuingizwa chupa watuhumiwa njia kuu Nani ameasisi? Hili halikubali.

**Polisi Babati kama kuna aliyehusika asimamishwe kupisha uchunguzi
 
View attachment 2823504
Hashimu Ally Phillemon, mkazi wa Babati Mjini anaeleza kwamba alikamatwa eneo lake la kazi, Paleii Lake View Garden, mali ya mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba na kupigwa, kujeruhiwa na kuwekewa chupa katika maeneo ya haja kubwa.

Hashimu Ally anadai, Pauline Gekul alitoa bastola, akamueleza achague kukalia chupa mwenyewe au apigwe risasi na mwili wake wakautupe katika Ziwa Babati. Alipogoma, wakampiga sana, wakamuingizia chupa sehemu ya haja kubwa.

Hashimu Ally anasema alituhumiwa na bosi wake (Pauline Gekul) kutumwa kuweka sumu ili kumuua Pauline Gekul, tuhuma ambazo hazijathibitishwa popote hata na jeshi la polisi, akasulubiwa sana kisha kukabidhiwa polisi Babati na kumpiga kila siku asubuhi na jioni, kwa siku nne.

Hashimu Ally anasema alikana tuhuma zote hizo akiwa kituo cha polisi Babati Mjini na hata chini ya mikono ya mateso ya Pauline Gekul. Baada ya kupigwa kwa siku nne mfululizo akiwa polisi Babati, alidhaminiwa na baba yake mzazi lakini baadaye akaitwa ofisi za Manyara ili kutoa maelezo.

View: https://m.youtube.com/watch?feature=shared&v=04BSzpoa6xo

Hata hivyo, Mbunge Pauline kupitia Katibu wake alikanusha taarifa hiyo katika ujumbe uliowekwa kwenye mitandao ya kijamii ukimtuhumu Hashimu kufanya udanganyifu na kushirikiana na washindani wa Pauline wa kibiashara kumfanyia ushirikina na baadaye ujumbe huo kufutwa kwa maelezo kuwa suala hilo liko mikononi mwa Polisi.

Kusoma zaidi kuhusu majibu ya pauline ingia >> Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Saa chache baada ya tuhuma hizi kusambaa na kupigiwa kelele na wadau mbalimbali ikiwemo wa JamiiForums, Rais Samia Suluhu, jioni ya tarehe 25 Novemba 2023, ametengua uteuzi wa Naibu Waziri huyo wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Zaidi soma >> Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Nina maswali
1.Hiko chakuka chenye sumu kilichukukiwa sampuli?
2.Je Gekul ana historia ya uhalifu na unyanyasaji.
 
Kazi ya shetani ni kuchinja kuua na kuahribu ukiendekeza ushirikina ipo siku utakurudi
 
Alichofanyiwa huyu kijana, huenda kinafanywa kwa watu wengi wakiwemo wale waliokuwa wanatekwa na watu wasiojulikana.

Na katika kulinda heshima zao katika jamii, wahanga hawa huchagua kukaa kimya kuliko kuesma hadharani vitendo walivyofanyiwa.

Kwa mtazomo huo, ni imani yangu hata waliomuingizia chupa makalioni kijana huyu katika tuhuma zinazomkabili Pauline Gekul, waliamini nae angekaa kimya. Hata hivyo, kwa huyu kijana ihali mekuwa tofauti kabisa otherwise wasingethubutu kufanya walichokifanya.

Ni wazi huu ushenzi unafanywa kwa watu wengi tu na ndio maana wakamfanyia na huyo kijana.

Unajiuliza kwanini wawaze kufanya hivyo kama hio sio ndio tabia yao?

Endapo haki itatendeka na tuhuma kuthibtishwa, kijana huyu ajiandae kulipwa fidia kubwa(adai fidia kubwa) na iwe somo kwa wengine

Mungu ana makusudi na kila jambo.
 
Alichofanyiwa huyu kijana, huenda kinafanywa kwa watu wengi wakiwemo wale waliokuwa wanatekwa na watu wasiojulikana.

Hivyo, katika kulinda heshima zao katika jamii, wahanga hawa huchagua kukaa kimya kuliko kuesma hadharani vitendo walivyofanyiwa.

Ni imani yangu, hata waliomuingia chupa makalioni kijana huyu katika tuhuma zinazomkabili Pauline Gekul, waliamini nae angekaa kimya. Hata hivyo, kwa huyu kijana imekuwa tofauti kabisa otherwise wasingethubutu kufanya walichokifanya.

Ni wazi huu ushenzi unafanywa kwa watu wengi tu na ndio maana wakamfanyia na huyo kijana.

Unajiuliza kwanini wawaze kufanya hivyo kama hio sio ndio tabia yao?

Endapo haki itatendeka na tuhuma kuthibtishwa, kijana huyu ajiandae kulipwa fidia kubwa(adai fidia kubwa) na iwe somo kwa wengine

Mungu ana makusudi na kila jambo.
Huyu mama kama kweli na Afa.
 
Back
Top Bottom