View attachment 2823504
Hashimu Ally Phillemon, mkazi wa Babati Mjini anaeleza kwamba alikamatwa eneo lake la kazi, Paleii Lake View Garden, mali ya mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba na kupigwa, kujeruhiwa na kuwekewa chupa katika maeneo ya haja kubwa.
Hashimu Ally anadai, Pauline Gekul alitoa bastola, akamueleza achague kukalia chupa mwenyewe au apigwe risasi na mwili wake wakautupe katika Ziwa Babati. Alipogoma, wakampiga sana, wakamuingizia chupa sehemu ya haja kubwa.
Hashimu Ally anasema alituhumiwa na bosi wake (Pauline Gekul) kutumwa kuweka sumu ili kumuua Pauline Gekul, tuhuma ambazo hazijathibitishwa popote hata na jeshi la polisi, akasulubiwa sana kisha kukabidhiwa polisi Babati na kumpiga kila siku asubuhi na jioni, kwa siku nne.
Hashimu Ally anasema alikana tuhuma zote hizo akiwa kituo cha polisi Babati Mjini na hata chini ya mikono ya mateso ya Pauline Gekul. Baada ya kupigwa kwa siku nne mfululizo akiwa polisi Babati, alidhaminiwa na baba yake mzazi lakini baadaye akaitwa ofisi za Manyara ili kutoa maelezo.
View: https://m.youtube.com/watch?feature=shared&v=04BSzpoa6xo
Hata hivyo, Mbunge Pauline kupitia Katibu wake alikanusha taarifa hiyo katika ujumbe uliowekwa kwenye mitandao ya kijamii ukimtuhumu Hashimu kufanya udanganyifu na kushirikiana na washindani wa Pauline wa kibiashara kumfanyia ushirikina na baadaye ujumbe huo kufutwa kwa maelezo kuwa suala hilo liko mikononi mwa Polisi.
Kusoma zaidi kuhusu majibu ya pauline ingia >>
Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana
Saa chache baada ya tuhuma hizi kusambaa na kupigiwa kelele na wadau mbalimbali ikiwemo wa JamiiForums, Rais Samia Suluhu, jioni ya tarehe 25 Novemba 2023, ametengua uteuzi wa Naibu Waziri huyo wa Wizara ya Katiba na Sheria.
Zaidi soma >>
Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji